Home » » DIWANI WA KATA YA VIJIBWENI (CCM), ATOA PIKIPIKI MBILI KWA AJILI YA KUSAIDIA UCHAGUZI WA VIONGOZI WA SERIKALI ZA MITAA

DIWANI WA KATA YA VIJIBWENI (CCM), ATOA PIKIPIKI MBILI KWA AJILI YA KUSAIDIA UCHAGUZI WA VIONGOZI WA SERIKALI ZA MITAA


 Diwani wa Kata ya Vijibweni, Suleiman Mathew (wa tatu kushoto), akimkabidhi ufunguo wa moja kati ya pikipiki mbili, Katibu  wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wa Kata hiyo, Salum Kabenza Dar es Salaam leo, alizozitoa kwa ajili ya kusaidia uchaguzi wa viongozi wa Serikali za Mitaa katika kata hiyo ambao unatarajiwa kufanyika Disemba 14, 2014(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com)

Wanachama wa CCM wa Kata ya Vijibweni wakiwa kwenye hafla hiyo ya makabidhiano ambayo ilikwenda sanjari na kuhamasishana kuhusu uchaguzi huo ambapo walisema ushindi ni lazima.


 Diwani wa Kata ya Vijibweni, Suleiman Mathew (wa tatu kushoto), akihutubia katika mkutano huo.
 Diwani Mathew akimkabidhi sh. 50,000 Katibu wa CCM, Tawi la Mkwajuni, Shaban Dololo kwa ajili ya kusaidia huduma mbalimbali katika ofisi yake.
 Diwani Mathew akimkabidhi sh. 50,000 Katibu wa CCM, Tawi la Upendo, Beatrice Bwana kwa ajili ya kusaidia kununulia vifaa vya ofisi kama karatasi na huduma nyingine za ofisini kwake.
Wanachama wa CCM wa Kata hiyo wakifuatilia matukio yaliyokuwa yakiendelea kwenye mkutano huo. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com)
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa