Home » » MAJI YA RUVU CHINI YAANZA KUTOKA DAR

MAJI YA RUVU CHINI YAANZA KUTOKA DAR

MAMLAKA ya Majisafi na Majitaka (DAWASCO) imesema baadhi ya maeneo katika Jiji la Dar es Salaam yameanza kupata maji baada ya kukamilika kuunganishwa kwa bomba la maji ya Mtambo wa Ruvu Chini.
Meneja Uhusiano wa Dawasco, Evalasting Lyalo alisema hayo jana wakati akizungumza na gazeti hili kuhusu baadhi ya maeneo kukosa maji tangu wiki iliyopita. Alisema hata hivyo tatizo hilo lilimalizika jana.
Maeneo yaliyoathirika ni Mji wa Bagamoyo, Mapinga, Bunju, Boko, Tegeta, Kunduchi, Salasala, Jangwani, Mbezi Beach na Kawe.
Maeneo mengine ni Mlalakuwa, Mwenge, Mikocheni, Msasani, Sinza, Manzese, Mabibo, Kijitonyama, Kinondoni, Oysterbay, Magomeni, Upanga, Kariakoo, Posta, Ilala, Ubungo Maziwa, Kigogo, Mburahati, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Buguruni, Chang’ombe na Keko.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Chanzo;Habari Leo

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa