Jokate na Guoxun wakionyesha mikataba baada ya kusaini
Jokate na Guoxun wakibadilishana mikataba baada ya kusaini.
Jokate
Mwegelo akizungumza katika hafla hiyo
Afisa
Mtendaji mkuu wa kampuni ya Rainbow Shell Craft Company Limited (CEO), Deng Guoxun akuzungumza katika hafla
hiyo
Jokate
akiteta jambo na Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa kwenye hafla hiyo
Wageni
mbalimbali waalikwa wakishughudia hafla hiyo
Meya
wa Manispaa ya Ilala akiteta jambo na Mbunge wa Viti maalum (CCM) Mariam
Kisangi katika hafla hiyo.
Dar es
Salaam. Mbunifu mavazi, Miss Tanzania wa namba mbili 2006, mwanamuziki na muigizaji wa filamu, Jokate
Mwegelo amesaini makubaliano yenye thamani ya Sh8.5 billion na kampuni ya
Kichina, Rainbow Shell Craft Company Limited
kwa ajili ya kuzalisha na kuuza bidhaa mbalimbali za lebo yake ya Kidoti.Makubaliano
hayo yalisainiwa leo kwenye hotel ya
Serena baina ya Jokate na Afisa Mtendaji mkuu wa kampuni ya Rainbow
Shell Craft Company Limited (CEO), Deng
Guoxun.
Akizungumza
katika hafla hiyo, Jokate alisema kuwa
makubaliano hayo ni ya kudumu na kampuni hizo mbili zitazalisha na kuuza bidhaa
za kidoti Tanzania nzima na nje ya mipaka yake.
Alifafanua
kuwa kampuni ya China itawekeza Tanzania na kuwafaidisha watanzania kwa kutoa
nafasi ya ajira. Alisema kuwa pia wanatarajia kujenga kiwanda ili kuinua uchumi
wa nchi na maisha ya watanzania.
“Hii ni hatua kubwa ya maendeleo kwangu, kama
unavyojua, wakati naanza kujishugulisha na masuala ya urembo, ubunifu na
uanamitindo, sikutegemea kufikia hatua hii ya kuingiza bidhaa zangu kimataifa,
lakini sasa, ndoto zangu zimetimia na najivunia mafanikio haya,” alisema
Jokate.
Alisema kuwa
mbali ya kutoa mitindo tofauti ya kisasa ya nguo, kampuni yake pia itazalisha
aina mbali mbali za viatu, nywele ikiwa pamoja na mawigi, weaving, Rasta na viatu vya wazi (sandals)
ambazo kwa sasa zipo tayari kwenye soko la Tanzania.
“Mpango
wangu ni kupanua soko la bidhaa zangu kama Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Afrika
Kusini na nchi nyingine za Afrika,” alisema.
Afisa
Mtendaji wa Guoxun alisema kuwa wamefurahi kukamilisha ubia na kampuni ya
Kidoti na haya ni matunda ya ushirikiano wa kudumu baina ya serikali yao na
Tanzania.
“Tumefurahi sana kukamilisha makubaliano haya,
tunatarajia kuongoza katika soko la hapa nchini na wenzetu (wachina)
watafaidika pia, ” alisema Guoxun.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment