Diwani wa CCM kata ya Magomeni, Julian Bujugo
Bujugo, aliwaambia wanahabari kuwa amefungua shauri la madai na mlalamikiwa ni Jumuiya ya Wazazi ya CCM.
Alisema hatua hiyo inatokana na jumuiya hiyo chini ya Mwenyekiti
wake, Abdallah Bulembo, ‘kumpora’ Chuo cha Kilimo na Mifugo Kaole cha
mjini Bagamoyo, ambacho ni mali ya jumuiya hiyo.
Hata hivyo, Bulembo amemkosoa Bujugo kwa hatua hiyo na kusema
aliwahi kufungua kesi kama hiyo iliyotolewa hukumu na Jaji John Utamwa
wa Mahakama Kuu na kutakiwa kulipa fidia ya Shilingi milioni 150.
Kwa upande wake, Bujugo alisema uporwaji wa chuo hicho ulifanywa
hivi karibuni na Bulembo akishirikiana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na
usalama ya wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, akiwamo Mkuu wa Wilaya,
Ahmed Kipozi.
Hivi karibuni, Bulembo alitangaza kukisimamisha chuo hicho kwa
madai kuwa mwendeshaji Bujugo, alibadili matumizi ya iliyokuwa shule ya
sekondari Kaole na kuanzisha chuo hicho bila ridhaa ya jumuiya hiyo.
Lakini Bujugo alisema (huku akionyesha nakala vivuli vya
makubaliano na malipo kati ya pande mbili hizo), kuwa jumuiya hiyo
imeshindwa kumheshimu badala yake kumvua Umeneja na uendeshaji wa chuo
hicho kwa mabavu.
Alisema katika hali iliyomstaajabisha, Bulembo akiwa na wajumbe wa
kamati ya ulinzi na usalama wilayani Bagamoyo, walimvua uendeshaji wa
chuo hicho na kukisimamisha.
Alidai kuwa makubaliano waliyoyafikia kati yao, ikiwa ni pamoja na
kuilipa jumuiya hiyo asilimia tano ya mapato yake, yalimuingizia
gharama zikiwamo za ujenzi na ukarabati wa majengo, maabara, vifaa,
mifugo na stahiki za wanafunzi na wafanyakazi ambavyo kiasi chake
kinakadiriwa kuwa Shilingi bilioni nne.
Akizungumzia sakata hilo, Bulembo alisema chuo hicho hakiwezi
kufunguliwa na badala yake kuwataka wazazi na wanafunzi kufuatilia madai
yao katika mamlaka husika ikiwamo kupitia kwa Afisa Elimu wa mkoa wa
Pwani.
“Bujugo ana majengo katika shule zake, anachapaswa kukifanya si
kusababisha hasara kwa wanafunzi na kuendeleza malumbano, awachukue
wanafunzi waliomlipa fedha awapeleke kwenye majengo yake ili wamalizie
kozi zao huko,” alisema.
Pia, Bulembo alitoa wito kwa serikali kupitia wizara ya elimu na
mafunzo ya ufundi, kufuatilia kwa akribu uendeshaji wa taasisi za elimu
nchini ili kuabaini na kudhibiti kasoro zinazochangia kuwaathiri
wanafunzi, walimu na wazazi.
CHANZO:
NIPASHE
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
KUELEKEA UCHAGUZI 2015: JE UNAPENDA NANI AWE KIONGOZI WAKO? JAZA FOMU HII FUPI HAPA
docs.google.com
docs.google.com
0 comments:
Post a Comment