Mwenyekiti
wa timu ya soka ya Simba Ismail Aden Rage amewataka wachezaji wa timu
hiyo kutokukata tamaa pamoja na kupoteza mchezo dhidi ya Mgambo ya
mkoani Tanga.
Ismail Aden Rage mmoja kati ya viongozi wa soka
anayeelekea kushabihiana kilugha na aliyekuwa waziri wa habari ya Iraq
enzi za utawala wa Sadam Hussein Ally-Sahaf amekutana na wachezaji wake
hii leo baada ya kupata kizunguzungu cha kipigo cha jeshi la mgambo ya
kabuku mkoani Tanga cha bao moya kwa 0.
Baada ya kipigo hicho kulikuwa na taarifa zisizo
rasmi yakuwa wachezaji hawajalipwa na wengine wakipienyeza mwalimu
Logarusic amekuwa mkali mno na mwenye kuwatolea wachezaji maneno
yasovikwa nguo. Ismail amekana nakuwapa kongole wachezaji wake huku
akasema Mgambo walijihami mno kwakurudi nyuma baada yakubahatisha goli.
Simba ilazamika kusafiri tena kuelekea mkoani Mbeya
kukabiliana na walimbukaji wa ligi Mbeya city siku ya Jumamosi katika
uwanja wa sokoine.
Chanzo:ITV Tanzania
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment