Viongozi
wakuu wa vyama vinavyuounda umoja wa katiba ya wananchi -UKAWA-
wamewataka wananchi wanaowaunga mkono umoja huo kutoshiriki katika zoezi
la kupiga kura ya maoni ya katiba inayopendekezwa linalotarajiwa
kufanya mapema mwezi aprili mwaka huu kutokana na mchakato mzima wa
kupatikana kwa katiba hiyo inayopendekezwa ulikuwa batili.
Akizungumza na waandishi wa habari, mwenyekiti wa mwenza wa umoja
huo Prof Ibrahimu Lipumba amesema UKAWA hawawezi kushiriki katika kura
ya maoni ya katiba inayopendekezwa ambayo haijapatikana katika misingi
ya kidemokrasia pamoja na ukiukwaji wa makubaliano ambapo awali kupitia
kituo cha demokrasia-TDC- walikubaliana na Mhe.Rais kwamba zoezi hilo
lifanyike baada ya uchaguzi mkuu wa rais na wabunge jambo ambalo
halikutekelezwa.
Kwa upande wake, mwenyekiti mwenza mweshimiwa Freeman Mbowe amesema
mpaka sasa ziko katiba pendekezwa zaidi ya nne mitaani, jambo
linalozidi kuwachanganya wananchi, na kusisitiza kuwa haiwezekani
daftari ya kudumu la wapiga kuwa tayari kabla ya mwezi aprili ambapo pia
ameitupia lawama tume ya taifa ya uchaguzi-NEC- kwa kuwashirikisha
wafadhili katika changamoto zilizojitokeza katika mfumo wa kupiga kura
kielektroniki badala ya kuwashirikisha wadau wakiwemo viongozi wa vyama
vya siasa.
Aidha mwenyekiti mwenza Bwana James Mbati amedai kushtushwa na
zoezi la kupiga kura ya maoni ya katiba pendekezwa linalotarajiwa
kufanyia mapema mwezi aprili wakati wananchi hawajapata elimu ya
kutosha, hakuna daftari la kudumu la wapiga kura sambamba na viongozi wa
vyama kutopatiwa katiba inayopendekezwa na kusistiza umoja huo sasa
umejiekeza zaidi katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi
oktoba mwaka huu.
Chanzo:ITV Tanzania
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment