Jeshi
la Polisi usiku wa kuamkia leo limekamata shehena ya nyaya za umeme
kwenye nyumba ya mkazi mmoja eneo la Nyeburu kata ya Majohe wilayani
Ilala.
Hatu ya kukamatwa na nyaya hizo imetokana na baadhi ya wasamaria
wema kuiarifu polisi baada ya kutilia shaka roli moja lililobeba nyaya
hizio katika nyumba ya mkazi huyo na kusafirishwa na ndipo polisi
ilipofika na kufanya ukaguzi ikazikuta rundo hilo huku mhusika akikimbia
na kuacha familia yake.
Meneja wa shirika la ugavi la umeme tawi la kisarawe madaraka
marumbo amesema ni wizi mkubwa ambao unashangaza kuona vifaa
vilivyokutwa hapo ni vingi vyenye kama ghala huku ikiwa na thamani
isiyopungua milioni 100 ambayo vinaweza kupelekwa kwenye mradi wowote.
Mwenyekiti wa mtaa huo wa Nyeburu Bw,Hamisi Gea amesema aliitwa na
polisi waliokuwa wakitaka kufanya upekuzi na alishangazwa kuona mkazi
huyo ana rundo la vifaa hivyo.
Hadi ITV ikiondoka eneo hilo tayari roli tatu za Tanesco ikiwamo
winchi ilikuwa ikipakia vifaa hivyo kwa ajili ya kuvipeleka polisi
Chanzo:ITV Tanzania
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment