Baraza
la Sanaa la Taifa (BASATA) linapenda kuwatangazia Wasanii na wadau wote wa
Sanaa nchini kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete kwa kifungu namba 5 (1) cha Sheria namba 23 ya mwaka 1984
iliyolianzisha Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) amemteua ndugu Godfrey Lebejo
Mngereza kuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).
Barua
ya Januari 16, 2015 iliyoandikwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Sihaba Nkinga imeeleza kwamba uteuzi wa Mngereza unaanza
Januari 23, 2015.
Kabla
ya Uteuzi huo Bwana Mngereza alikuwa Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA kwa
kipindi cha kutoka Februari 2013 hadi 2015 mwanzoni akitokea Idara ya Utafiti
na Stadi za Wasanii ya BASATA aliyokuwa akiiongoza kama Mkurugenzi wake.
Godfrey
Mngereza ni msomi mwenye shahada ya uzamili (MA) katika masuala ya Sanaa kutoka
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na amepata kuwa Mwalimu wa Chuo Kikuu hicho katika
Idara ya Sanaa na Sanaa za Maonesho (FPA) hadi mwaka 2008 alipoajiriwa rasmi na
BASATA kama Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Habari ambayo kwa sasa
inafahamika kama Idara ya Utafiti na Stadi za Wasanii. Aidha, shahada yake ya kwanza ilikuwa katika
masuala ya Sanaa aliyoipata kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Sanaa
ni kazi, tuipende na kuithamini
Imetolewa na Kitengo cha Habari- BASATA
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment