Meja Generali Joseph Kapwani.
Hali hiyo inatokana na kuongezeka kwa mashirika zaidi ya 40 yaliyosajiliwa nchini kuratibu shughuli za usafiri wa anga.
Hayo yamesemwa jana na Meja Generali Joseph Kapwani, Mkuu wa
Kamandi ya Jeshi la Anga aliyemwakilisha Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na
Usalama, aliyekuwa mgeni rasmi katika sherehe za uwekaji wa jiwe la
msingi wa Hanga la Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) na maadhimisho
ya miaka ya 40 ya chuo hiko.
Jenerali Kapwani alisema kuanzishwa kwa jengo hilo ambalo litakuwa
la kwanza nchini Tanzania kutoa kozi ya uhandisi wa kutengeneza ndege
na urubani ni jambo jema na hatua kubwa na muhimu ya kimaendeleo kwa
taifa.
Alisisitiza kuwa uanzishwaji wa kozi hiyo ya utaongeza wataalamu
na kuimarisha ufanisi wa kiutendaji sambamba na kukuza uchumi wa taifa
kwani wadau wengi na watumiaji wa huduma za usafiri wa anga watanufaika.
“Ili anga liwe salama linahitaji kuwepo na vyombo imara kama ndege
ambazi ubora wake unategemea sana utaalamu wa wahandisi waliofunzwa
vizuri na kuielewa vyema fani hiyo.” alisema Generali Kapwani.
Mkuu wa chuo hiko, Dk. Zacharia Mganilwa, alisema kuwa sekta ya
anga ni nyeti katika uchumi wa nchi, ikisimamiwa vizuri kwa kuwa na
wataalamu wenye weledi, inaweza ikaongeza kwa kiasi kikubwa pato la
taifa.
Aliongeza kuwa upande wa marubani wazawa kwa Tanzania idadi
hairidhishi kutokana na takwimu zinazoonyesha kuwa mpaka Juni, 2014
Tanzania ilikuwa na marubani 533 na kati ya hao, 239 ni wazawa na
waliobakia 294 ni wageni.
CHANZO:
NIPASHE
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment