Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.
Ukawa, ambayo ilianzishwa wakati wa mkutano wa Bunge Maalumu la
Katiba Februari, mwaka jana, inaundwa na vyama vya Chadema, CUF,
NCCR-Mageuzi na NLD, ambavyo vimetiliana saini makubaliano ya
kushirikiana katika chaguzi zote.
Afisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene, alisema jana kuwa ajenda
hizo zitajadiliwa katika kikao maalumu kilichoitishwa na Kamati Kuu ya
Chadema, jijini Dar es Salaam kwa dharura leo.
Alisema Kamati Kuu inatarajia kuibuka na maamuzi mazito katika kikao hicho.
Ajenda nyingine ni pamoja na uandikishaji wa daftari la kudumu la
wapigakura kwa kutumia mfumo mpya wa kielektroniki wa BVR, ambao ufanisi
wake umegubikwa na utata mwingi.
Nyingine ni mchakato wa kura ya maoni ya wananchi kuamua ama
kuikubali au kuikataa rasimu ya katiba inayopendekezwa kutokana na
sheria yake kukiukwa na hivyo, kufanya uwezekano wa kutekelezwa kwa
matakwa ya sheria Aprili, mwaka huu, kama ilivyotangazwa na serikali
kuwa ndoto.
Alisema ajenda hizo zitajadiliwa na baada ya kupokea taarifa kutoka
kwa wataalamu, wakiwamo wanasheria pamoja na sekretarieti ya chama
hicho kabla ya kuibuka na maamuzi mazito.
CHANZO:
NIPASHE
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment