Home » » TANESCO: TATIZO LA LUKU TAYARI TUMEDHIBITI

TANESCO: TATIZO LA LUKU TAYARI TUMEDHIBITI

Mkurugenzi Mtendaji Tanesco, Felchesmi Mramba.
Shirika la Umeme Nchini (Tanesco), limesema leo litamaliza tatizo la umeme kwenye mfumo mzima wa kutolea miamala ya luku kutokana na kutokea hitilafu za kiufundi kwa siku tatu mfululizo.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Naibu Mkurugenzi  wa Tanesco, Decklan Mhaiki, alisema shirika lake linaomba radhi kwa usumbufu huo uliojitokeza.

“Tunaomba radhi kwa usumbufu huo na kwamba kwa sasa tatizo limeshashughulikiwa kwa asilimia 70(jana) na hadi kufikia kesho (leo) tatizo hilo loitakuwa limekamilika kwa asilimia 100…mafundi  wetu wanaendelea  na matengenezo ili kumaliza kero hiyo,” alisema Mhaiki.

Naye Meneja Mwandamizi wa Tehama (ICT), Kusenha Mazengo, alisema tatizo hilo lilikuwa katika mifumo ya kusambaza umeme wa luku kwenda kwa mawakala wanaosambaza kwa wateja wa kawaida.

“Wateja wetu walikosa huduma hiyo kutoka kwa mawakala kutokana na hitilafu ya mfumo huo, “ alisema Mazengo.
Mapema Januari 10, mwaka huu mfumo wa luku ulishindwa kufanyakazi na kusababisha baadhi ya watu kukosa huduma ya nishati hiyo.
CHANZO: NIPASHE

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa