Meneja wa Vipindi wa East Africa Radio, Nasa
Kingu (katikati), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam jana kuhusu kampeni ya kuhamasisha vijana inayojulikana kama
`Zamu
Vijana
nchini wameandaliwa kampeni ya kuwahamasisha na kuwaelimisha kwa ajili
ya kushiriki katika upigaji kura ya maoni ya Katiba inayopendekezwa na
uchaguzi mkuu mwaka huu.
Kura ya maoni ya kukubali au kuikataa Katiba inayopendekezwa
itafanyika Aprili 30, mwaka huu na uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika
Jumapili ya mwisho ya Oktoba, mwaka huu.
Kampeni hiyo itwayo `Zamu yako 2015' imeandaliwa na Kituo cha
Runinga cha EATV na Redio ili kuwaelimisha vijana kujiandikisha katika
daftari la wapigakura, kupigia kura ya maoni ya Katiba inayopendekezwa
na uchaguzi mkuu wa kuwachagua madiwani, wabunge na rais.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkuu
wa vipindi vya EATV na Redio, Nasser Kingu, alisema kuwa katika
kuhakikisha lengo lao linatimia, vituo hivyo vitatumia vipindi na
matanagazo mbalimbali kwa kuwahusisha wadau ambao watatoa elimu kuhusu
umuhimu wa vijana kushiriki katika upigaji kura ya maoni ya Katiba
inayopendekezwa na uchaguzi mkuu.
“Kupitia vipindi vyetu na matangazo, tunaamini kwa kiasi kikubwa
itasaidia vijana kufahamu mambo mazuri yaliyomo katika Katiba
inayopendekezwa na kupiga kura kuchagua viongozi wanaofaa kwa maisha yao
na watoto wao,” alisema Kingu.
Kingu alisema wameamua kufanya kampeni hiyo kwa kuwa imebainika
kuwa katika taifa lolote duniani, vijana ndilo kundi kubwa linaloweza
kuchochea mabadiliko ya haraka.
Aidha, alisema takwimu za Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012,
zinaonyesha kuwa vijana wenye umri wa miaka 18 kwenda juu, wana sifa ya
kushiriki kupiga kura wakati Watanzania takriban 22,424,136 wakitarajiwa
kushiriki katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Alisema kati ya idadi hiyo, vijana kuanzia miaka 18 hadi 40 ambao ni asilimia 68.20 ya Watanzania wenye sifa ya kupiga kura.
Aliongeza kuwa hii si mara ya kwanza kwa EATV kuandaa kampeni hiyo
kwani mwaka 2010 kituo hicho kiliandaa kampeni iliyojulikana kama
‘Kijana acha kulalamika tumia kura yako kuleta mabadiliko’, ambayo
alisema hata hivyo, haikufanikiwa kutokana na kuanza kuhamasisha badala
kutoa elimu kwanza.
CHANZO:
NIPASHE
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment