Home » » JK AKABIDHIWA RASMI UENYEKITI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

JK AKABIDHIWA RASMI UENYEKITI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI


Rais Kikwete amerejea nyumbani mara baada ya mkutano huo ambao umehudhuriwa na Marais wa nchi zote tano za Jumuiya na Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini ambaye amehudhuria kama mualikwa maalum katika kipindi hiki ambapo mazungumzo ya awali ya kuijadili nchi yake kama inaweza kupata uanachama katika EAC yanaendelea. Pichani ni Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Profesa Mark Mwandosya akimkaribisha Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki , Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya Rais kuwasili katika uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere akitokea Nairobi Kenya ambapo alihudhuria mkutano wa kilele wa wakuu wa nchi Jumuiya ya Afrika Mashariki.Kushoto ni Waziri wa Elimu na Mafunzo Dkt.Shukuru Kawambwa
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wao Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya pamoja na Rais Yoweri Museveni wa Uganda, Rais Paul Kagame wa Rwanda na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakizungumza chemba kabla ya kuingia kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa  Kenyatta International Convention Center(KICC)Nairobi,Kenya  katika mkutano wa kawaida wa 16 wa Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki uliofanyika Ijumaa Februari 20, 2015
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wao Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya pamoja na Rais Paul Kagame wa Rwanda kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa  Kenyatta International Convention Center(KICC)Nairobi,Kenya  katika mkutano wa kawaida wa 16 wa Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki uliofanyika Ijumaa Februari 20, 2015
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Naibu Rais wa Kenya, Mhe. William Rutto na maafisa wengine wakiwa kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa  Kenyatta International Convention Center(KICC)Nairobi,Kenya wakati wimbo wa Taifa wa Tanzania katika mkutano wa kawaida wa 16 wa Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki uliofanyika Ijumaa Februari 20, 2015
Kutoka kushoto ni mgeni mwalikwa, Rais wa Sudani Kusini, Mhe Salva Kiir, Rais wa Burundi, Mhe Pierre Nkurunziza, Rais Jakaya Mrisho Kikwete(Tanzania),Rais Uhuru Kenyatta(Kenya)Rais Yoweri Museveni (Uganda) Rais Paul Kagame (Rwanda) na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Balozi Dk Richard Sezibera wakiwa kwenye ukumbi wa mikutano kwenye  mkutano wa kawaida wa 16 wa Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki
Rais Jakaya Mrisho Kikwete(kushoto)akipokea bendera ya Afrika Mashariki(EAC)kutoka kwa Rais wa Kenya,Uhuru Kenyatta ikiwa ni ishara ya kumkabidhi rasmi Uenyekiti wa  EAC  kwenye  mkutano wa kawaida wa 16 wa Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki uliofanyika Ijumaa Februari 20, 2015 katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi. Picha na IKULU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa