Utoaji wa vitambulisho vya taifa unaendelea jijini Dar es Salaam ambapo
Father Kidevu Blog ilitembelea moja ya kituo cha kutolea vitambulisho
hicho kilichopo Ilala Bungoni na kukuta umati wa watu ukisubiri kupatiwa
vitambulisho vyao. Katika eneo hilo kuna mitaa mbalimbali wengi ikiwa
ni kutoka maeneo ya Vingunguti, Buguruni hadi Ilala mchikichini. Watu wa
Pugu na maenweo ya Gongo la Mboto na Vitongoji vyake pia wanaendelea
kupatiwa vitambulisho hivyo.
Wananchi wakisubiri kupatiwa vitambulisho vyao.
Mama huyu tayari ameshapata kitambulisho chake.
Kutokana na foleni iliyopo wakazi hawa wameamua kukaa chini kusubiri
watu wapungue. Licha ya zoezi hilo kuendelea lakini baadhi ya watu
wamelalamikia utaratibu wake wa kuwaleta watu kutoka maeneo ya mbali na
badala yake watu hao wangekuwa wakienda katika maeneo yale yale
waliyoandikishiwa.
CREDIT:FATHER KIDEVU
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment