Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa akizungumza kwenye ofisi ya gazeti la Jambo leo ikiwa sehemu ya ziara yake kwenye vyombo vya habari.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndg. Nape Nnauye amesema CCM haiwezi na wala haina mpango wa kupoteza historia ya mahali ilipozaliwa TANU.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na
wahariri wa gazeti la JamboLeo siku ya Ijumaa tarehe 6 februari 2015 alipotembelea ofisini kwao katika ziara
ya kutembelea vyombo mbalimbali vya habari nchini.
Alisema kumekuwa na maneno mengi kama vile ukarabati unaofanywa kwenye ofisi ndogo ya CCM Lumumba ni kupoteza historia ya TANU.
Alisema
kinachofanyika ni maboresho ya ofisi ndogo ya CCM Lumumba ifanane na
hadhi, mahitaji na wakati wa Chama hicho, lakini historia itabaki kama
kielelezo cha Mahala ilipozaliwa TANU.
Alifafanua
kuwa awali ofisi ya mwanzo ilikuwa nyumba ya udongo iliyoezekwa kwa
makuti, kisha ikaondolewa makuti na kuezekwa mabati ya madebe,baade
ikabadilishwa na kuwekwa bati za kisasa.
“Historia
ya TANU iliyopo kwenye jengo la Lumumba, tutaendelea kuitunza na
hatutoibomoa kwani ni kielelezo cha tulikotoka na tunajivunia historia
hiyo, tutaitunza”
Alisema kama tusingefanya
maboresho maana yake tungekuwa na jengo la udongo ambalo limeezekwa
makuti mpaka leo. Akadai wanaolalamika hawajui historia ya eneo hilo,
ila akawashukuru kwa mapenzi yao mema kwa Chama hicho.
Aliongeza
kuwa hakuna namna CCM itaruhusu historia ifutike na huku ikiendelea
kuhifadhi historia za vyama vingine, hasa bile vya ukombozi kusini mwa
bara la Afrika.
Nape pia alikanusha uvumi kuwa
CCM inawekeza kitega uchumi eneo hilo, akasema wanakarabati ofisi na
itakuwa ofisi sio kitega uchumi.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment