Na
Benedict Liwenga, Maelezo-Dar es Salaam.
WAZIRI wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe amelipongeza Kanisa la
Wasabato (SDA) kwa kuwa mfano mzuri wa ustahimilivu, uvumilivu wa kidini na
imani katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mhe. Membe ameyasema hayo
leo wakati alipokuwa akifunga rasmi Kongamano la siku 4 (4-7 Februari, 2015) Kimataifa la Utume kwa Kanisa la Sabato
lililofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambalo lilishirikisha
Mataifa zaidi ya 20 Duniani.
Alisema kuwa, katika kipindi chote cha uongozi wake kama Waziri
hajawahi kusikia mgogoro wala matatizo yakioongozwa na SDA dhidi ya madhehebu
mengine ya dini hapa nchini na hata dhidi ya wananchi.
“Mpo mnafanya kazi zenu, mnachapa shughuli zenu kwa amani na utulivu,
hamjachokoza mtu na hiyo ni sifa ya dini mojawapo yenye amani duniani”, alisema
Mhe. Membe.
Alisisitiza kwa kuwataka wananchi wa dini zote nchini kuiga mfano wa
wana SDA ili Tanzania iendelee kuwa nchi yenye amani na utulivu.
Aidha, alieleza kuwa, Dini na Diplomasia vina husiana pale
masuala ya amani, ulinzi na usalama yanapoguswa huku akiwataka wananchi wa dini
zote nchini kushiriki katika kutengeneza viongozi bora katika jamii kwa misingi
ya uadilifu ambao watasimamia amani na kujiepusha na vitendo viovu ikiwemo
rushwa.
Aliongeza kuwa dhamira
ya Serikali ya kuendelea kushirikiana nalo kwa ajili ya ustawi wa nchi huku
akieleza kuwa, Serikali itaendelea kulinda uhuru wa kuabudu kwa dini zote kama
inavyoelezwa kwenye Katiba ya Jamhuriu ya Muungano wa Tanzania.
Naye Rais wa Baraza
Kuu la Makanisa ya Sabato Duniani, Askofu Ted Wilson alisema kuwa anawaombea
Viongozi wa Tanzania waendelee na maono kwa lengo la kuwatumikia
wananchi na kwamba wakimtumaini Mungu atawawezesha kupata maono mapya kwa
ajili ya kulitumikia Taifa zima.
Kongamano hilo lilishirikisha
Mataifa zaidi ya 20 ambapo Kanisa hilo la Wasabato ni Kanisa linalokua duniani
likiwa na Waumini milioni 307 huku Waumini milioni 30 wakiwa Afrika na takriban
milioni 5 wakiwa Tanzania.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment