Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
aziri Mkuu, Mizengo Pinda
akisalimiana na Balozi wa Brazil nchini, Fransisco Carlos Soares Luz
amabaye alikwenda ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Aprili
29, 2015 kuaga.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
akizungumza na Balozi wa Brazil nchini, Fransisco Carlos Soares Luz
amabaye alikwenda ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Aprili
29, 2015 kuaga.
………………………………………………………………….
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda
amekutana na Balozi wa Brazili nchini Tanzania, Bw. Fransisco Luz na
kujadiliana mambo kadhaa kuhusu maendeleo na mahusiano baina ya nchi
hizo mbili.
Akizungumza na Balozi Luz ofisini
Magogoni jijini Dar es Salaam leo mchana (Jumatano, Aprili 29, 2015),
Waziri Mkuu alimshukuru Balozi huyo kwa ushirikiano ambao ameutoa kwa
Serikali ya Tanzania katika kipindi cha miaka sita ambacho amekuwa
akiiwakilisha nchi yake hapa nchini.
Balozi Luz ambaye amepangiwa
kwenda Jordan kwenye kituo kipya, alisema anaondoka nchini akiamini
kwamba mtu atakayekuja kumpokea ataendelea mambo aliyoyaanzisha ikiwemo
mradi wa kufadhili utafiti na uendelezaji wa zao la pamba kwenye kituo
cha utafiti wa kilimo cha Ukiriguru, Mwanza.
Balozi Luz ambaye alifika kumuaga
Waziri Mkuu, alitumia fursa hiyo kumweleza Waziri Mkuu kwamba ubalozi
huo umefanikiwa kupeleka Watanzania wawili kusomea kozi za Uzamili
(Masters’ Programme) kwenye vyuo vikuu vya Brazil.
“Wanafunzi hawa wawili waliondoka
Februari mwaka huu, ni kati ya wanafunzi saba waliofuzu lakini wengine
watano walikosa ufadhili kutoka kwenye taasisi zao. Mmoja anasomea Geo-Physics na mwingine Oil Engineering,” alisema Balozi Luz.
Balozi Luz ambaye anatarajia
kuondoka nchini mapema mwezi ujao, amepangiwa kituo kingine ambapo
ataenda kuiwakilisha nchi yake nchini Jordan.
IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
- L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM
JUMATANO, APRILI 29, 2015.
0 comments:
Post a Comment