Home » » MAOFISA BOT WA WANA KESI YA KUJIBU.

MAOFISA BOT WA WANA KESI YA KUJIBU.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Benki Kuu Tanzania (BoT).
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imesema maofisa wanane wa Benki Kuu Tanzania (BoT) akiwamo Justina Mungai, wana kesi ya kujibu dhidi ya mashtaka 14 ya kughushi na kuwasilisha vyeti vya kidato cha nne vilivyoghushiwa.
 
Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Nyigulila Mwaseba, alitoa uamuzi huo jana baada ya upande wa Jamhuri kufunga ushahidi wao.
 
Hakimu Mwaseba alisema baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na  mashahidi wa Jamhuri bila kuacha shaka washtakiwa wana kesi ya kujibu na kwamba wanatakiwa kupanda kizimbani kujitetea dhidi ya mashitaka yanayowakabili Juni 16 hadi 17, mwaka huu.
 
Mbali na Mungai, washtakiwa wengine ni Christina Ntemi, Siamini Kombakono, Janeth Mahenge na Beatha Masawe, Jacquiline Juma, Philimina Mutagurwa na Amina Mwinchumu.
 
Septemba 19, mwaka 2008, upande wa Jamhuri uliwasomea washtakiwa hao mashitaka yao .
 
Ilidaiwa kuwa siku isiyofahamika mwaka 2001, jijini Dar es Salaam, mshtakiwa Mungai alighushi cheti cha kidato cha nne, chenye namba S.342/43 kilichotolewa Februari 26, 1980.
 
Aidha, ilidaiwa kuwa cheti hicho kilitolewa na Baraza la Mitihani la Taifa.
 
Katika shtaka la pili, mshtakiwa huyo anadaiwa kuwa siku isiyofahamika mwaka 2001, jijini, aliwasilisha cheti hicho huku akijua ni cha kughushi.
 
Katika shtaka la tatu na nne, ilidaiwa kuwa siku isiyofahamika mwaka 2002 jijini, mshtakiwa wa pili alighushi cheti cha kidato cha nne chenye namba za usajili  S.0222/42 kikionyesha kimetolewa Novemba 26, mwaka 1999 na kwamba aliwasilisha BoT.
 
Katika shtaka la tano na sita, ilidaiwa kuwa siku isiyofahamika mwaka 2001 jijini Dar es Salaam, mshtakiwa Kombakono, alighushi cheti cha kidato cha nne chenye namba za usajili S.238-0076 kilichotolewa Machi 14, mwaka 1997 akionyesha kuwa kimetolewa na Baraza la Taifa ambapo walikiwasilisha BoT.
 
Katika shtaka la saba na nane, mshtakiwa wa Mahenge, anadaiwa kuwa alighushi cheti cha kidao cha nne, chenye namba za usajili S.311/0071 kikionyesha kimetolewa Machi 14, mwaka 1997,  na Baraza la Taifa ambapo aliwasilisha BoT.
 
Aidha, shtaka la tisa na kumi, ilidaiwa kuwa siku isiyofahamika jijini, mshtakiwa Massawe, anadaiwa kuwa 2001 benki kuu, alighushi  cheti cha kidato cha nne, chenye namba za usajili S.331/0071 kikionyesha kimetolewa Aprili 22, mwaka 2000, na Baraza la Taifa ambapo alikiwasilisha BoT.
 
Ilidaiwa kuwa, shtaka la 11 na 12, mshtakiwa Juma, anadaiwa kuwa siku isiyofahamika mwaka 2000 jijini, alighushi cheti cha kidato cha nne chenye namba za usajili S.375/020 kikionyesha kimetolewa Machi 14, mwaka 1999 na Baraza la Taifa ambapo alikiwasilisha BoT.
 
Pia, shtaka la 13 na 14, mshtakiwa Mutagurwa anadaiwa kuwa siku isiyofahamika mwaka 2002, alighushi cheti cha kidato cha nne, chenye namba za usajili S.0764/0012 kikionyesha kimetolewa Machi 14, mwaka 1997 na Baraza la Taifa ambapo alikiwasilisha BoT. 
 
Katika shtaka la 15 na 16, mshtakiwa Mwanchungu anadaiwa kuwa siku isiyofahamika, 2001 jijini, alighushi cheti cha kidato cha nne, chenye namba za usajili S.0307-004 kikionyesha kimetolewa Machi 28, mwaka 1991 na Baraza na Taifa, ambapo aliwasilisha  BoT. 
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa