Home » » TMA: MVUA DAR ZIMEFIKA UKINGONI.

TMA: MVUA DAR ZIMEFIKA UKINGONI.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
mamlaka ya hali ya hewa tanzania (tma)
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema mvua zilizoanza kunyesha Machi hadi Mei, mwaka huu na kusababisha athari mbalimbali, ikiwamo vifo, upotevu wa makazi na uharibifu wa miundombinu katika Jiji la Dar es Salaam zimefikia ukingoni.
 
Mkurugenzi wa Huduma wa Utabiri wa hali ya Hewa (TMA), Dk. Hamza Kabelwa, alisema kwa sasa mvua zitaendelea hadi Mei 20, mwaka huu, lakini katika mikoa ya Pwani Kaskazini inayojumuisha mikoa ya Pwani, Tanga, na visiwa vya Unguja na Pemba.
 
“Kwa jana na leo, vituo vya maeneo hayo havijasoma mvua. Kituo cha Pemba Mei 16, mwaka huu, kilisoma mvua milimita 35, huku kwingine ikiendelea kupungua…taarifa zetu tunazichukua kwa siku kumi. Kwa sasa tunakusanya taarifa ya siku kumi zijazo na tutaiweka wazi kwa ajili ya umma kujua,” alisema.
 
Alisema kwa wakazi wa Dar es Salaam, mvua zimekwisha na kwamba, zitakazoendelea kwenye maeneo mengine hazitakuwa na kasi kama iliyokuwa Mei 6 na 7, mwaka huu. 
 
Dk. Kabelwa alisema kwa sasa wanafanyia uchambuzi wa mifumo ya hali ya hewa ili kuona hali ya mvua ikoje.

CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa