Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Wizara
ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), imetahadharisha kuwapo na
matukio machache yenye dalili za uhalifu uliopitiliza mipaka
yanayohusisha kuua wanajeshi pamoja na polisi.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi,
aliliambia Bunge jana, wakati akiwasilisha bajeti ya wizara hiyo kwa
mwaka 2015/16.
Alisema licha ya hali ya usalama wa taifa kuwa ya kuridhisha kuna
matukio kama hayo ya kuwaua askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania
(JWTZ) na polisi na kuwapora silaha vituoni akisema ni udhihirisho wa
uhalifu uliopitiliza.
Akizungumzia usalama mipakani alisema ni shwari japo kwa upande wa
Magharibi wahalifu wenye silaha wanaodhaniwa kutokea Congo na Burundi,
walivamia, kushambulia na kupora wavuvi kwenye Ziwa Tanganyika na
Victoria.
Kwa upande wa mipaka Kusini alieleza kuwa licha ya kwamba kuna
mgogoro baina ya Malawi na Tanzania kuhusu mpaka wa Ziwa Nyasa eneo hilo
liko salama .
WASIOKWENDA JKT KUBANWA
Waziri aliliambia Bunge kuwa idadi ya waliojiunga na JKT katika
mwaka 2014/15 ni 40,082, hata hivyo, aliwaonya wale ambao hawakwenda kwa
mujibu wa sheria wataendelea kuhesabika kama watoro.
“Wito wangu kwa vijana ni kushiriki mafunzo haya kwani ni ya mujibu
na kwa wale ambao hawakushiriki bila ridhaa yetu wataendelea kuwa
kwenye orodha yetu ya vijana watoro,” aliliambia Bunge.
KUZALISHA MILIPUKO
Akizungumzia uzalishaji jeshini alisema Shirika la Mzinga,
linakusudia kuanzisha kiwanda cha milipuko pamoja na kituo cha utafiti
wa zana za kivita.
Waziri wa Ulinzi alisema pamoja na kuanzisha vituo hivyo Mzinga
itasimika mfumo wa usalama wa kielektroniki katika kiwanda hicho.
Alisema shirika hilo katika mwaka wa fedha wa 2014/15 liliendelea
kukamilisha ujenzi wa kiwanda cha kuzalisha risasi na kukarabati na
kujenga maghala mapya ya silaha.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment