Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Siku
moja baada ya wafanyabiashara wenye ulemavu wa soko la Mchikichini
jijini Dar es Salaam kufunga barabara baada ya kubomolewa meza za
biashara zao, serikali imewaruhusu kuendelea na kazi eneo hilo huku
ikifanya tathmini ya hasara iliyopatikana.
NIPASHE Jumamosi ilishuhudia jana meza za wafanyabiashara hao zilizovunjwa usiku wa kuamkia juzi zikijengwa upya.
Wafanyabiashara hao juzi walilazimika kufunga barabara ya Kawawa na
Uhuru kwa saa sita baada ya kukuta meza zao za biashara zikiwa
zimevunjwa.
Akizungumza na gazeti hili jana, mmoja wa wafanyabiashara hao
ambaye anayejihusisha na uuzaji wa mabegi sokoni hapo, Mfaume Seleman,
alisema kuwa viongozi wao walipokea barua kutoka kwa Mkurugenzi wa
Manispaa ya Ilala.
Alisema barua hiyo imewataka waendelee kufanya shughuli zao katika maeneo waliyotoka au walipokuwa wakifanya biashara zao.
Alisema barua hiyo imeeleza kuwa, Serikali imeliona tatizo hilo na
kulifanyia kazi kwa kufanya uchunguzi kwa kushirikiana na uongozi wa
wafanyabiashara hao.
Seleman alisema kuanzia jana viongozi wao wameanza kukutana na serikali kufanya vikao ili kupata ufumbuzi wa kudumu.
Barua hiyo ambayo NIPASHE imeona inaeleza kuwa, uchunguzi
unafanyika na itakapobainika nini kilijiri kwa waathirika Halmashauri ya
Ilala itakaa na waathirika ili kuweza kubaini hasara walizopata na
fidia kufanyika.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment