Home » » AFB wapokea dola milioni 20 kupanua uwekezaji kusini mwa Jangwa la Sahara

AFB wapokea dola milioni 20 kupanua uwekezaji kusini mwa Jangwa la Sahara

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 



Gemcorp Capital LP (“GEMCORP”) yawekeza dola za kimarekani mil 20 kwa afb Mauritius Ltd
Dar es Salaam, Tanzania: Juni 4 2015 ….Kampuni ya Huduma za Kifedha ya afb, ambayo inajihusisha na kutoa ushauri na huduma za kifedha kwa wajasiriamali, imeingia  mkataba wa dola za Kimarekani mil 20 na  kampuni ya GEMCORP, inayojihusisha na uwekezaji wenye mtazamo wa msuala ya kimasoko.
Akizungumzia mkataba huo, Mkurugenzi wa afb Karl Westvig alisema, “Nimefarijika sana kuingia makataba huu ambao umekuja kwa wakati muafaka ambao pia ni muhimu sana kwa kampuni. Uwekezaji huu wenye mantiki kutoka kwa GEMCORP utatoa mchango mkubwa sana katika kuleta maendeleo kusini mwa Jangwa la Sahara.” 
Kwa sasa afb ipo pia katika mataifa ya Ghana, Kenya, Zambia na Tanzania, huku ikiwa na mpango wa kujitanua katika nchi nyingine za Afrika  ifikapo mwaka  2020, ikiwa na bidhaa zenye  ubunifu na ufumbuzi wa hali juu yenye kukidhi vigezo vyote sokoni.
Kwa mujibu wa ripoti ya Benki kuu ya Dunia, zaidi ya watu milioni 400 waliopo kusini mwa jangwa la Sahara bado wanafanya shughuli zao nje ya mfumo rasmi wa kifedha. “afb inalenga kutoa huduma rahisi za kifedha kwa watu ambao wamekuwa nje ya mfumo, kwa kufanya hivyo kutawarahisishia kuboresha maisha yao,” Westvig aliongeza.
Akizungumzia juu ya uwekezaji huo, Mkurugenzi wa GEMCORP Atanas Bostandjiev, alisema: “Huduma za kifedha ni sekta muhimu sana kwa mustakabali wa kampuni yetu na tumekuwa tukiangalia hasa soko la Afrika, afb ni fursa kubwa sana ya kiuwekezaji kwetu. Ikiwa na lengo la kutekeleza maendeleo ya kifedha kupitia ufumbuzi wa kiteknolojia, kampuni hii inalenga katika kuharakisha ukuaji wa maendeleo kulingana na mahitaji ya bara la Afrika hasa kwa tabaka la kati.”
“Kwa kiasi kikubwa tunaithamini na kuiheshimu dhamira ya GEMCORP kwa afb na imani yao kwa dira yetu na mikakati ya kampuni yetu,” alisema  Westvig. “ Naamini tutaendelea kufanya kazi kwa pamoja na kuendeleza ushirikiano kwa maendeleo ya  afb.” Alisema.





Notes to Editors:
About afb Mauritius Limited
afb is a financial services company providing innovative consumer and SME credit products in sub-Saharan Africa. Committed to responsible lending, afb is the first to offer mass-market, voluntary repayment products in the markets in which it operates. These products are delivered through technology-based solutions in partnership with mobile network operators, retail stores and other enterprises. afb has over 600,000 customers in Kenya, Ghana, Zambia and Tanzania, and over 450 retail partners.
For more information visit www.afb.com or follow afb on Twitter @afbAfrica.
About GEMCORP Capital
Gemcorp Capital LLP (“GEMCORP”) is an investment management firm focused on Emerging Markets. It invests through private debt, public debt, equity and macro strategies. The firm is headquartered in London and has offices in Africa and Asia. It is authorised and regulated by the Financial Conduct Authority in the United Kingdom.
For more information visit www.gemcorp.net
Contacts:
Sonali Das
afb
PR & Communications
sonali@afb.com
+254 712 436088

Steffan Williams / Mike Turner
Finsbury (advisers to GEMCORP)
GEMCORP@finsbury.com
+44 207 251 3801

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa