Home » » KONGAMANO LA JUMUIYA YA WAFANYABIASHARA TANZANIA(TANZANIA BUSINESS ENTREPRENEURS) WENGI WANUFAIKA‏

KONGAMANO LA JUMUIYA YA WAFANYABIASHARA TANZANIA(TANZANIA BUSINESS ENTREPRENEURS) WENGI WANUFAIKA‏

 Mwenyekiti wa Tanzania Business Entrepreneurs for Women Haika Lawere akizungumza na Waandishi wa Habari
 
 Kutoka Kulia ni Getrude, Haika Lawere, Hilda Mgaja na  Julieth mjale wakiwa katika pozi wakati wa Kongamano hilo.
 Mmoja wa wawezeshaji Bwana James Mwang'amba akiendelea kutoa mada juu ya Ujasiliamali
 Muwezeshaji Chriss Rupia akitoa maelezo juu ya namna ya kuanzisha Kampuni na hatua mbalimbali ambazo mtu anaakiwa zifuata wakati wa kufungua Kampuni hasa Binafsi.
 Mwenyekiti wa Tanzania Business Entrepreneurs for Women Haika Lawere(wa kwanza Kulia) pamoja na wadau wengine wakitembelea baadhi ya Meza wakati wa kongamano hilo lililofanyika Mbezi Garden Hotel
 Wa kwanza kulia ni moja wa majaji  wakiwa akiangalia baadhi ya meza ambazo watu wamefanya kazi kwa ubunifu wao wenyewe
 Baadhi ya wajasiliamali na wadau mbalimbali wakiwa katika Kongamano
 Getrude (Kulia) akiendelea kuchukua kumbukumbu ya wadau waliofika katika kongamano
Hawa ni wale waaalam wa Virutubisho Tiba ambavyo ni Bora kabisa na kwa hakika Kutoka Alliance wakionesha Bidhaa zao zilizo katika ubora wa Juu, hapo utapata mambo kibao ikiwa ni pamoja na Kuongeza kumbukumbu kwa kichwa chako na mambo kibao.. Wasiliana nao sasa kwa namba 
+255 653 691 138
Dada huyu anafanya vizuri sana  vizuri sana anatengeneza mwenyewe kila kitu Mfollow Instagram @getrudemembe
Baadhi ya wajasiliamali wakionesha kazi zao...
 Wanaitwa Ricada Bags and shoes wanapatikana Mtaa wa Nangurung'ombe/Congo Kariakoo , Hawa ni wauzaji wa Viatu bora vya wanawake pamoja na Bags za aina kibao, usipitwe na Fasheni Cheki nao sasa kupitia namba yao ya simu +255 787 670 483  au wafollow instagram @rithermassao
 Wanaitwa Coco Cosmetics and Beauty hawa wanavipodozi na unyunyu wa maana unaweza Check nao kupitia +255712082506
Chek nao hao unapohitaji kuwa na Afya njema zaidi   Wasiliana na namba hizi 0653685085 
au 0715 033204
 Hawa jamaa ni Sheeedah sana.... watakudizainia, maneno, picha katika sehemu unapotaka unataka jua zaidi cheki nao hapa 0717 515036
 Kicheko Huja chenyewe hasa kama Bidhaa unayouza au mnunuzi ni noma.... cheki Raba hizi ni nouma. huyu anauza mambo Original kabisa.. hebu Mgongee Simu sasa 0658015040
Wanaitwa JNHM Unique Weddings hawa watakudizainia Mavazi ya Harusi na Sherehe mbalimbali pia hawa ni Wataalam wa mambo mengi zaidi Gonga hapa 0754347083
Mambo ya watoto wazazi Mpo? Pamoja na mengine mengi kazi kwenu Glowrgeous Beauty Studio  Cheki nao hapa 0713 469 780
 Tukio linaendelea
 Elimu inaendelea ....
Akisaini katika kitabu cha Wageni
Umati wa watu wakiwa wanatazama Bidhaa mbalimbali katika Kongamano hilo. 
Picha na Fredy Anthony.

Story na  Dotto Mwaibale
WAJASIRIAMALI wanawake nchini wametakiwa kuwa na moyo wa uthubutu ili kupiga hatua ya maisha na kiuchumi badala ya kuwa waoga.
Mwito huo umetolewa na Mratibu wa Kongamano la Jumuia ya Wafanyabiashara Wanawake Tanzania, Julieti Mjale wakati akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kongamano hilo lililofanyika Hoteli ya Mbezi Garden Dar es Salaam jana.
"Uthubutu katika jambo lolote ni muhimu kwani unamfanya muhusika kupiga hatua ya maendeleo" alisema Mjale
Alisema wajasiriamali waliowengi wamekuwa na mipango mizuri ya kubuni biashara fulani lakini wanakuwa na hofu ya kupoteza fedha zao na hiyo inatokana na kushindwa kuthubutu au kuchukua maamuzi magumu ya kuanza kufanya biashara waliyoikusudia.
Akijitolea mfano yeye alisema alithubutu kwa kuanza kufanya biashara za chini lakini leo hii ana nyumba za kupangisha na kufikia hatua ya kufanya biashara za kwenda nje ya nchi na kuandaa makongamana ya namna hiyo kwa ajili ya kutoa elimu ya biashara.
Mwenyekiti wa Jumuia hiyo, Haika Lawere alisema lengo la kongamano hilo ni kuwakutanisha wajasiriamali wanawake ili kupeana uzoefu wa biashara na kujua changamoto walizonazo na kuzitafutia ufumbuzi pamoja na kupanua wigo wa shughuli zao na kutafuta masoko mapya ya bidhaa zao.
Katibu wa Jumuia hiyo, Hilda Ngaja, alisema changamoto kubwa waliyonayo wajasiriamali wanawake ni kutokuwa na uelewa mkubwa wa kufanyabiashara zao na kujikuta wakirudi nyuma kimaendeleo na ndio maana wamekuwa wakitumia fursa za semina na makongamano kwa ajili ya kuelimishana. (Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com-simu namba-0712-727062)
 

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa