Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Anitha
Jonas – MAELEZO.
Serikali
yafikia muafaka katika mgogoro wake na wafanyabiashara juu ya matumizi ya mashine za kieletroniniki
EFD’s.
Hayo
ameyasema jana Waziri wa Fedha Mhe.Saada
Mkuya alipokuwa akitoa taarifa
hiyo kwa vyombo vya habari juu ya Serikali kufikia muafaka wa makubaliano yaliyofanyika kwa ushirikiano
wa Kamati kuu ya Taifa iliyoshirikisha
wajumbe kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na Viongozi wa Jumuiya
ya wafanyabiashara katika ngazi ya Taifa.
“Matumizi
ya mashine za EFD yalipoanza yalileta changamoto kwa wafanyabiashara ,hivyo niliunda kamati ya
kitaifa pamoja na kamati katika ngazi za Mikoa na Wilaya pamoja na wenyeviti
wakuu wa mikoa kutafuta suluhu la suala hili”alisema Mhe.Mkuya.
Waziri
Mkuya aliendelea kusema Kamati imetoa mapendekezo mbalimbali kwa Serikali
ikiwemo ya muda mfupi ambayo wameshaanza kuyafanyia kazi na mengine ni yakisera
ambayo yatahitaji muda mrefu yatafuata utaratibu unaopaswa katika utekelezaji wake,kwa
ufuatiliaji na ushirikiano wa karibu,kupitia kamati ya Kitaifa itakayodumu kwa
kipindi cha miaka miwili.
Naye
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara nchini Bw.Johnson Minja aliipongeza
serikali kwa kubali kukaa meza moja na wafanyabiashara katika kutatua mgogoro huo
uliyokuwepo katika matumizi ya mashine za EFD na kuakukubali kupokea changamoto
za wafanyabiashara na kuahidi kuzifanyia kazi.
“Serikali
imekubali kupitia mfumo wa utozwaji kodi kuanzia ngazi ya bandarini na kuongeza uwazi ilikuleta uelewa kwa
wafanyabiashara na kuepuka kutozwa kodi kubwa kutoka na kukosa uelewa wa
gharama za ulipaji kodi”,alisema Bw.Minja.
Aidha
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo ya wafanyabiashara aliendelea kusema ni wajibu wa kila mmoja kulipa kodi na
hii ni kwa maendeleo ya nchi na pia ni kosa kwa mfanyabiashara yoyote kuendesha
biashara yake bila kuwa na namba ya utambulisho wa mlipakodi (Tin Number),tunataka namba ya
walipakodi iendelee kuongezeka na kuondoa kabisa wafanyabiashara wasio lipa
kodi.
Mbali na hayo nae Kamishana
Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Rished
Bade aliipongeza kamati kwa kuweza kufika mwafaka na kuweza kuzitambua
changamoto mbalimbali zilizokuwa zikiwasumbua wafanyabiashara na ameahidi ,kuwa
ofisi yake itaendelea kuwawajibisha watu
wote wanao kiuka taratibu za
0 comments:
Post a Comment