Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Burundi Women and Girls Movement, Prof Christine Mbonyingingo (kati) akizungumza na wanahabari.
Rais wa Taasisi ya Coalition of Civil Society for Election Monitoring, Justine Nkurunziza akifafanua jambo.
Mwanasheria kutoka nchini Burundi, Janvier Bigirimana akijibu maswali ya wanahabari. Kushoto ni Prof. Christine Mbonyingingo
Wanaharakati
pamoja na taasisi mbalimbali za kutetea haki za binadamu kutoka nchini Burundi
zimewataka marais wa umoja wa nchi za afrika mashariki (EAC) kutumia nguvu za
kijeshi kumng’oa rais anayegombea muhula wa tatu nchini humo kinyume na katiba
ya nchi hiyo, Pierre Nkurunziza.
Wakizungumza
na waandishi wa habari leo hii katika ukumbi wa Hoteli ya New Africa jijini
Dar, wanaharakati hao kutoka Taasisi ya Civil Society na Burundi Women and
Girls Movement, walisema kuwa wameamua kufikia hatua ya kuomba msaada wa
kijeshi kutokana na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaofanya na jeshi la
nchini humo.
Wanaharakati
hao ambao wameweka kambi yao nchini Tanzania walidai kuwa kutumika kwa nguvu ya
kijeshi kutoka nchi jirani shirikisho la Nchi za Afrika Mashariki ndiyo
suluhisho pekee la kurejesha amani nchini humo huku akiwataka marais wa nchi
hizo jirani na Burundi kutoyafumbia macho mateso ya raia wa Burundi.
Mbali
na hayo wanaharakati hao walidai kusikitishwa na kitendo cha wanaharakati
wenzao wa Burundi kuzuiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
jijini Dar na kutakiwa kuondoka mara moja nchini japo kuwa walikuwa na nyaraka
zote za kusafiria.
0 comments:
Post a Comment