Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Ndugu
 wananchama wa Chama cha Mapinduzi-CCM ni wiki mbili tangu tulipo maliza
 mchakato ndani ya chama kumpata mgombea wa Urais hapo Octoba 25, 2015. 
Kwa
 mara ya kwanza wananchama 41 waliomba kuteuliwa na chama. Hii 
inaonyesha kwamba demokrasia imekuwa ndani ya chama. Kati ya wanachama 
wa CCM waliochukua fomu alikuwa ni mheshimiwa waziri mkuu mstaafu Ndugu 
Edward Lowasa. Utaratibu wa chama ulifuatwa ili kumpata mgombea ikiwa ni
 pamoja kamati ya maadili, kamati kuu na halmashauri kuu ya taifa na 
mkutano mkuu. Katika mchakato pia chama kilitumia idara mbalimbali kama 
usalama wa taifa, takukuru na tume ya maadili ya umma kupata taarifa 
mbalimbali kuhusu wagombea hasa za uadirifu, usalama wan nchi na 
kadhalika.
Baada
 ya mchakato kumalizika baadhi ya wagombea na wanachama hawakuridhika na
 matokea, katika chama kikubwa kama CCM haizekani wanachama wote 
wakaridhika na maamzi. Ndugu wanachama na watanzania tunaomba kuelewa 
kuwa kumpata kiongozi mkubwa wa nchi kama Rais siyo kazi rahisi. Baadhi 
ya wanachama ambao hawakuridhika na maamzi ya chama ni Ndugu Edward 
Lowasa, amekuwa akizungumza nje ya chama kuhusu kutotendewa haki na 
baade kuhama chama na kujiunga na chamacha demokrasia na 
maendeleo-CHADEMA.
Kwa nini Ndugu Lowasa hakuteuliwa kuwa mgombea wa CCM?
Ndugu
 wanachama na watanzania, Mheshimiwa Lowasa alijenga hisia na kuamini 
kuwa ndani ya CCM wagombea wote walistahili kuenguliwa isipokuwa yeye. 
Hii siyo demokrasia, baada ya kupitia repoti mbalimbali Ndugu LOWASA 
alienguliwa kwa sababu zifuatazo:-
1. Kukiuka taratibu za chama kwaani alionekana kufanya kampeni badala ya kutafuta wadhamini
2.
 Kutoa rushwa kwa wanachama mbalimbali hivyo kukigawa chama na kama 
angepishwa kuwa mgombea CCM ilikuwa katika hatari ya kuwekewa pingamizi 
mahakamani lakini pia angeweka watu wake kwenye utawala kuwalipa 
fadhira.
3.
 Edward Lowasa aliwahonga wajumbe katika uchaguzi wa wajumbe NEC 
uliofanyika miaka iliyopita ili kupata watu wake ndani ya NEC.
4.
 Kuanza kampeni kabla ya wakati, alikuwa akisafirisha watu mbalimbali na
 kuwalipa fedha nyingi kisha kutoa taarifa kuwa walikuwa wakimtaka 
kugombea Urais, hii ni hadaa na hatari kwa chama.
5. Kuwa na kashfa nyingi za ufisadi na matumizi mabaya ya ofisi ya umma akiwa waziri.
6.
 Kusemwa semwa kuhusika kuhusika na tuhuma za kutumia watu kudhuru 
baadhi ya watanzania na viongozi, hili lipo kwenye vyombo vya dola kwa 
uchunguzi, uchunguzi ukikamilika sheria itachukua mkondo wake.
7. Utajiri na mali usiokuwa na maelezo alizipataje kama vile kumiliki majumba nje ya nchi kama uingereza, singapole na nk.
Mwisho
 chama kimesikitishwa sana na kauli kuwa amekuwa akionewa na kusingiziwa
 kuwa alihusika na kashfa ya RICHMOND, ndugu wanachama kashfa ya 
RICHMOND ilianzia bungeni, CCM haikuhusika na kumwondoa kwenye uwaziri 
mkuu, lakini kwa kuwa imekuwa inajengeka kuwa alionewa tunaviomba vyombo
 vya sheria kulipeleka jambo hili mahakamani ili kuondoa dhana 
inayojengeka kuwa serikalia ya CCM inaonea wanachama wake. Doa 
linalotakwa kujengeka litapatiwa ufumbuzi na iwapo inathibitika kulikuwa
 na njama binafsi wote waliohusika kulidanganya bunge watachukuliwa 
hatua na chama lakini pia sheria itachukua mkondo wake.
Imetolewa na :-
Nape M.Nnauye
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA
ITIKADI NA UENEZI
 
 
 
1 comments:
CCm Organs ?
to qoute Nape;;; "Katika mchakato pia chama kilitumia idara mbalimbali kama usalama wa taifa, takukuru na tume ya maadili ya umma kupata taarifa mbalimbali kuhusu wagombea hasa za uadirifu, usalama wan nchi na kadhalika"
Post a Comment