Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Meneja Mauzo na Masoko wa Kampuni ya
Nuebrand EC, Cathreen Bukuku (kushoto), akizungumza katika mkutano na
waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu kongamano la wiki
ya huduma za kifedha na uwekezaji litakalofanyika Agosti 28 hadi 30
mwaka huu, viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Kulia ni
Mkufunzi na Mratibu wa Mipango wa Kampuni hiyo, Daniel Wadelanga.
Kongamano hilo limeandaliwa na Kampuni ya Nuebrand EC.
Mjumbe wa Timu ya Mauzo wa Benki ya Uba
United Bank for Africa, Tesha Filemon (katikati), akizungumza katika
mkutano huo kuhusu kazi mbalimbali zinazofanywa na benki hiyo.
Meneja wa Tawi la Kariakoo wa Benki ya
The Peoples Bank of Zanzibar Ltd, Badru Idd (wa pili kushoto),
akizungumza katika mkutano huo kuhusu benki hiyo na matawi yake.
Ofisa Usanifu Bidhaa na Usimamizi wa
Sharia Amana Benki, Jaffari Kesowani (kulia), akizungumza na wanahabari
kuhusu kazi mbalimbali zinazohusiana na na benki hiyo.
Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Jubilee Life Insurance, Adam Samson Namuhisa (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.
Msimamizi wa Masoko wa Kampuni ya Avic
Town, Daniel Kure (kulia), akielezea kadhi kadhaa zinazofanywa na
kampuni hiyo katika mkutano huo. Kushoto ni maofisa wa kampuni hiyo.
Meneja Masoko na Uhusiano wa Kampuni ya
Covenant Bank, Mhina Semwenda (kulia), akizungumzia shughuli
zinazofanywa na benki hiyo.
Wadau mbalimbali kutoka taasisi za kifedha wakiwa
kwenye mkutano huo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Wapiga picha wakiwa kazini. "Chezea kazi wewe"
Mmoja wa wanufaika na makongamano hayo yanayotolewa na Kampuni hiyo ya Nuebrand EC, Alphonce Mkubwa kutoka Mbeya akieleza faida ya makongamano hayo aliyoshiriki kwa zaidi ya miaka mitano sasa.
Na Dotto Mwaibale
TAFITI zinaonesha asilimia kubwa ya watu
hawatumii njia zilizo rasmi za kifedha kutokana na kukosa elimu ya
masuala ya kifedha na uwekezaji.
Hayo yamesemwa Dar es Salaam leo na
Meneja Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Nuebrand, Cathreen Bukuku wakati
akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu kongamano la
wiki ya huduma za kifedha na uwekezaji litakalofanyika Agosti 28 hadi
30 mwaka huu, viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam ambalo
litahusisha watu wote, wawe wajasiriamali au si mjasiriamali una
biashara au huna na wawekezaji wote ambapo washiriki watatoa kiingilio
cha ada sh. 2000/- kwa ajili ya kushiriki kongamano hilo ambapo watapata
cheti cha ushiriki,"alisema Bukuku.
Alisema lengo la kongamano hilo ni
kuweka uelewa katika masuala ya kifedha kwani watanzania wengi wamekuwa
hawatumii njia zilizosalama na rasmi za kifedha katika uwekaji, akiba na
kutengeneza mazingira kuhusiana na huduma za kibenki pamoja na
ujasiriamali.
Bukuku alisema washiriki watapata elimu
ya uelewa wa bima mbalimbali kama za maisha, afya na bima ya mali,
kupata elimu ya jinsi ya kuandaa mchamganuo mzuri wa biashara, kujifunza
ujuzi mbalimbali na kupata fursa ya kushiriki katika shindano la
kuandaa mchanganuo wa biashara ambapo atashinda fedha itakayomsaidia
kuanzisha au kuendeleza biashara yake.
Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Jubilee Life Insurance, Adam Samson Namuhisa,
alisema lengo lao ni kutoa elimu ya bima za maisha kwa watanzania na
kujua haki zao pamoja na kujua fursa zilizopo huku mshiriki akipata
huduma myimgi kwa wakati mmoja.
Mshindi wa kongamano hilo msimu
uliopita, Alphonce Mkubwa aliwataka vijana kujitokeza kushiriki ili
wapate elimu ya kufanya biashara ili wapate mafanikio," Nilikuwa mshindi
katika kutoa wazo la biashara ambapo nilishinda zabuni ya ukusanyaji
ushuru katika halmashauri ya Wilaya ya Chunya...huu ni muda wa kufanya
kazi kwani huu ni ukombozi kwa kutokukaa kijiweni,"alisema Mkubwa.
0 comments:
Post a Comment