Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
NA BEATRICE LYIMO
MAELEZO
Dar Es Salaam.
Ofisi ya Mkemia Mkuu wa
Serikali imewataka wadau wote wanaojihusisha na usafirishaji na uuzaji wa
kemikali kujisajili kabla ya hatua za kisheria hazijachukuliwa dhidi yao.
Kauli hiyo imetolewa
leo jijini Dar es salaam na Mkemia Mkuu wa Serikali Prof. Samwel Manyele wakati
wa warsha ya siku moja iliyolenga kuwaelimisha wadau wa uuzaji na usafirishaji kuhusiana
na usimamizi wa kemikali hatari na zenye madhara kwa afya na mazingira kwenye
maeneo ya bandari na wakati wa usafirishaji.
Amefafanua kuwa Sheria
ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali za Viwandani na Majumbani Na. 3 ya mwaka
2003 inawataka wadau kusajiliwa ili kuhakikisha kuwa kemikali zinatumika katika
hali iliyosalama wakati wa kusafirishwa,kuuzwa na kuhifadhi.
“Katika kuendelea kuimarisha utekelezaji wa
Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali za Viwandani na Majumbani, Wakala
wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali umekuwa ukifanya jitihada kadhaa
kuhakikisha wadau wote wanauelewa wa kutosha kuhusiana na maswala ya sheria”
alisisitiza Prof. Manyele
Alisema kuwa Ofisi ya
Mkemia Mkuu wa Serikali imekuwa ikijitahidi kutoa elimu kwa wadau kupitia
warsha, mikutano, ukaguzi, kushiriki kwenye maonyesho, mafunzo kwa wasimamizi
wa shughuli zinazohusiana na masuala ya kemikali na madereva wanaosafirisha
kemikali ili kuhakikisha kuwa wadau na wananchi wanatumia kemikali katika hali iliyosalama
kwao na mazingira.
Mbali na hayo warsha
hiyo imewakutanisha wadau muhimu wa Bandari kwa lengo la kupeana elimu na
kujadili juu ya namna bora ya kusimamia upakiaji, upakuaji, na uhifadhi wa shughuli
yeyote inayohusu kemikali hatari katika maeneo ya Bandari.
Aidha Mkemia Mkuu huyo wa
Serikali alisema kuwa Ofisi hiyo inaanda warsha nyingine ya kuelimisha wadau
juu ya kuchukua taadhari juu ya kujikinga na tukio ambalo linaweza kutokea
kutokana na mlipuko wa kemikali kama ilivyokea nchini China
0 comments:
Post a Comment