Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » CT Scan mpya iliyopelekwa muhimbili ilitolewa hospitalini Dodoma

CT Scan mpya iliyopelekwa muhimbili ilitolewa hospitalini Dodoma

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Serikali imekiri kwamba CT Scan mpya iliyonunuliwa kuziba pengo la kuharibika kwa iliyokuwepo katika hospitali ya Muhimbili Dar es salaam ilitolewa hospitali ya Benjamin Mkapa Ultra modern Hospitali mkoani Dodoma
Hayo yamebainika leo katika ukumbi wa bunge mjini Dodoma baada ya Mbunge wa jimbo la Chemba Juma Nkamia CCM kuuliza swali kwanini serikali imeamua kuchukua mashine ya CT Scan katika hospitali inayohudumia wagonjwa Dodoma na kuipeleka Muhimbili ina maana serikali ina lengo la kuwaua wananchi wa Dodoma.?


Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Khamisi Kigwangalla amesema kwamba serikali ilichukua uamuzi huo baada ya mashine hiyo kukosa jengo la kuifunga Mkoani Dodoma ambapo wakati huo huo hospitali ya Muhimbili imekuwa ikiwa inakumbwa na matatizo makubwa ya wagonjwa kukosa huduma hiyo.

''Mheshimiwa mwenyekiti kwa kuwa hospitali ya Benjamin Mkapa Ultra modern ilipata mashine hiyo lakini jengo lao bado halikamilika hivyo serikali imeandaa utaratibu wa kununua mashine mpya kwa ajili yao ili jengo lao likikamilika liweze kupata mashine mpya'' Ameeleza Dkt.Kigwangalla.


0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa