Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MKE wa Rais, Mama Janeth Magufuli amesema Serikali itaendelea
kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha wazee na watu
wasiojiweza wanapata huduma zote muhimu kwa kadri ya uwezo wake.
Aliyasema hayo jana Dar es Salaam wakati alipofanya ziara yake ya
kwanza ya kikazi katika Kituo cha makazi ya wazee na watu wenye ulemavu
cha Nunge, Kigamboni katika Manispaa ya Temeke na kuwakabidhi zawadi ya
vyakula.
“Serikali ina wajibu mkubwa katika kuhudumia wazee na watu
wasiojiweza lakini mtakubaliana kuwa serikali pekee haiwezi kumaliza
matatizo yote yanayowakabili watu hawa. Hivyo sote kwa pamoja tuna
wajibu wa kusaidia nguvu za serikali katika kuwahudumia wenzetu hawa,”
alisema.
Alisema kwa kulitambua hilo ametoa mchele kilo 3,000, unga kilo 3,000
na maharage kilo 1,200, ambavyo kulingana na idadi yao kila mmoja
amepatiwa kilo 25 za mchele, kilo 25 za unga na kilo 10 za maharage.
“Sote tunafahamu kuwa wazee na watu wasiojiweza wanahitaji upendo,
kuthaminiwa na kusaidiwa na kipimo kimoja wapo cha kupima jamii
iliyostaarabika na inayoheshimu misingi ya utu ni kuangalia namna
inavyowathamini wazee na watu wasiojiweza,” alieleza mke huyo wa Rais
Magufuli.
CHANZO : HABARI LEO.
0 comments:
Post a Comment