Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Raymond Mushumbusi, MAELEZO
Serikali
ipo kwenye mpango wa kuunda Mamlaka ya Mapato Kuu ya Taifa nje ya
Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) iliyopo kwa sasa ili kuondokana na
malalamiko ya kero za kodi kwa wananchi wenye kipato cha chini.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Kaimu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Alphayo Kidata alipokuwa akifafanua
kuhusu juhudi za Serikali katika kuwasaidia wananchi wa kipato cha
chini kuweza kumudu kulipa kiwango cha kodi kinachowekwa na na Mamlaka
hiyo.
“
Napenda kuwambia umma wa watanzania kwamba Serikali ya Awamu ya tano
inawajali watu wake na ndio maana imeona kuwa kuna haja ya kuunda Mamlaka
moja ya utozaji wa kodi itakayojumuisha taasisi zote zinazohusika na
kukusanya mapato nje ya kodi na ushuru ili kuondokana na malalamiko
mengi ya wananchi juu ya utozaji wa kodi hasa katika Halmashauri
zetu”Alisema Kidata.
Kamishna
Kidata amesema kuwa katika dunia hii hakuna Serikali ambayo
imechaguliwa na wananchi ikaamua tu kuwakandamiza wananchi wake katika
jambo lolote lile hivyo basi kwa sasaserikali ipo katika
mchakato wa kuunda Mamlaka hiyo ambayo itasaidia kuweka viwango vya
kodi ambavyo wananchi wa hali ya chini watamudu kulipa kutokana na
biashara au kazi wanazozifanya.
Kamishna
huyo ameongeza kuwa Mamlaka yake kwa kushirikiana na mamlaka nyingine
zinazokusanya kodi katika Halmashauri nchini watahakikisha wanalipatia
ufumbuzi suala la kero ya kodi kwa wananchi wa hali ya chini kwa kupata
muafaka ambao utasaidia pande zote mbili bila kukandamiza upande wowote
iwe Serikali ama mwananchi wa kawaida.
Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) imekuwa na rekodi nzuri ya ukusanyaji wa kodi
ila kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kuhusu kodi ambazo
zimekuwa kero na hazina tija. Hivyo Serikali imejipanga kuiongezea nguvu
Mamlaka hiyo kwa kuipa uwezo wa kukusanya na mapato ambayo hayatokani na kodi toka katika wizara, mashirika,tasisi za serikalina Halmashauri zote nchini.
0 comments:
Post a Comment