Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imefuta kodi elekezi kwa bidhaa zinazoingizwa nchini kwa msamaha wa kodi hususani zile zinazotoka nchini China kwa kuwata wafanyabiashara wanaoagiza na kuingizi bidhaa kutoka huko kulipa kodi inayotakiwa.
Hayo
yamesemwa leo na Kaimu Kamishna wa TRA, Alphayo Kidata alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari katika utaratuibu wa kuongea na umma
kwa kuwapa taarifa kuhusu makusanyo ya kodi ya kila mwezi.
Kaimu Kamishna huyo
amesema kuwa Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania imeamua kufuta
kodi elekezi ambayo ilikuwa inawapa punguzo la kodi wafanyabiashara
wanaoagiza na kuingiza bidhaa toka nchini China kwa kupunguziwa sehemu
ya kodi.
“Tumeamua
kuondoa kodi elekezi kwasababu haina faida kwa taifa letu kwani
inawanyima wafanyabiashara wengine ambao hawaagizi bidhaa kutoka China
fursa ya kushindana kibiashara na Serikali yetu sio ya kibaguzi ndio
maana tumaeamua kufuta kodi hii ili kuleta usawa kwa wafanyabiashara wote nchini”Alisema Kidata.
“Suala
liliopo kwa sasa ni kwa kila mwananchi anayepaswa kulipa kodi katika
kitu anachokifanya alipe kodi na atutafumbia macho ukwepaji wa kodi na
hakuna kitu kinachoitwa kodi elekezi wala msamaha wa kodi katika
Serikali hii, tulipe kodi kwa maendeleo ya taifa letu” aliongeza Kidata.
Aidha,
Kamisha Kidata amesema kuwa hakuna Sheria yoyote inayosema kuwa
kutakuwa na kodi elekezi ama msamaha wa kodi kwa mfanyabiashara yoyote
yule bali ule ulikuwa ni utaratibu tu uliowekwa na Mamlaka na baada ya kuona hauna umuhimu wala faida katika nchini yetu ikaamriwa ufutwe.
Katika
kusisitizi suala la kufutwa kodi elekezi na utekelezaji wake Kaimu
Kamishna wa kodi za Ndani toka TRA, Salum Yusuf amesema watalisimamia
suala la ulipaji kodi na yeyote atakayekaidi kulipa kodi kwa Mamlaka
husika watawachukulia hatua za kisheria na kusisitiza kuwa kulipa kodi
ni jukumu la kila mtanzania katika kuleta maendeleo ya taifa letu.
Mamlaka
ya Mapato Tanzania imekuwa na rekodi nzuri ya ukusanyaji wa kodi tangu
mwezi Desemba mwaka 2015 kwa kukusanya zaidi ya shillingi trillioni 1 na
wanaendelea na kasi ya kukusanya kodi zaidi na kwa takwimu zilizopo
kuanzia mwezi Julai mwaka 2015 mpaka mwezi Februari mwaka huu
wamekusanya jumla ya shillingi trillioni 8.6 ikiwa ni asilimia 99 ya
malengo waliojiwekea.
0 comments:
Post a Comment