Mwenyekiti wa kampuni ya Altalab Factories Group, kutoka Misri, Bw.Abdelhkim Altalab (kushoto) akitoa maelezo kwa mmoja wa wageni waliotembelea katika banda hilo kwenye maonyesho hayo.
Banda la bidhaa za Kiboko Alu-Zinc
Mwanadada Sarafina Wasley akitoa maelezo namna ya bidhaa zinazosambazwa na StoneBlock Bulding wakati wa maonyesho hayo.
Mwanadada Sarafina Wasley akitoa maelezo namna ya bidhaa zinazosambazwa na StoneBlock Bulding kwa wateja (hawapo pichani) wakati wa maonyesho hayo,
Meneja Masoko wa TCL (Technical Chemical Laboratory) , Bw Louay Abd El-Rahman (kushoto) akitoa maelezo kwa mgeni aliyetembelea banda hilo kwenye maonyesho hayo leo Mei 28.2016, katika ukumbi wa Mlimani City. (Picha zote na Andrew Chale,Modewjiblog).
Maonyesho
ya bidhaa z Plastiki yaliyoanza jana Mei 27.2016 katika ukumbi wa
Mlimani City, Jijini Dar es Salaam yanatarajia kufikia tamati hiyo kesho
Jumapili ya Mei 29.
Maonyesho
hayo ambayo Tanzania ni mwenyeji kwanza ya bidhaa za plastiki,
mpira, kemikali za petrol na ujenzi yanakuwa ya kipekee huku watu
mbalimbali wameendelea kujitokeza kwa wingi katika ukumbi wa Kituo cha
Mikutano cha Mlimani City jijiniDare s Salaam.
Awali
Meneja Mkuu wa Expo One, Ahmed Barakat ambao ni waandaaji wa maonyesho
hayo, alisema nchi zote za Afrika Mashariki na kati zinashiriki katika
maonesho hayo.
Afrika
–PPB-EXPRO ni jukwaa la kipekee la bidhaa mpya na yatatoa mwanya wa
kuyaelewa masoko yake ambayo hayafahamiki vizuri.
“Maonesho haya yamebuniwa kwa lengo la kukuza umoja miongoni mwa
Waafrika kwa kuimarisha mahusiano ya kibiashara kati ya Misri na
Tanzania na hali kadhalika kuyaweka masoko yake kwenye ramani ya
Afrika,kubainisha kuwa Tanzania ni ya kwanza katika orodha ya nchi za
Afrika ambapo Africa-PBB-EXPO imepanga kushirikiana nayo.
Alisema
kupitia Aramex na kwa uratibu wa TanTrade na Taasisi ya Sekta Binafsi
Tanzania (TPSF), Africa-PBB-EXPO inatoa fursa ya kipekee kwa waoneshaji
walio na kanzidata za kina kusajiliwa mara zinapopokelewa.
Barakat
alitoa wito kwa wafanyabiashara kushiriki katika maonesho hayo ili
kuweza ‘kubaini fursa za ushirikiano katika masoko haya mapya pamoja na
mtandao ulio na wateja na wenza wa kibiashara.
“Kampuni ya EXPO ONE ambayo ni mwandaaji, ni taasisi ya kati ya
usimamizi wa mikutano na maonesho ambayo imejikita katika kuandaa na
kutoa huduma kwa maonesho ya biashara ya kimataifa pamoja na
kuyatangaza mabanda ya Misri katika maonesho ya ndani na ya kimataifa.
0 comments:
Post a Comment