Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli amemteua Mhe. Jaji Shabani Ally Lila kuwa Jaji wa Mahakama
ya Rufani.
Kabla ya uteuzi
huo Mhe. Jaji Shabani Lila alikuwa Jaji
Kiongozi.
Uteuzi huu umeanza
leo tarehe 30 Mei, 2016.
Wakati
huo huo, Rais Dkt. Magufuli amemteua Mhe. Anne Semamba
Makinda kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).Uteuzi wa Mhe. Anne
Semamba Makinda ambaye ni Spika Mstaafu
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umeanza tarehe 25 Mei, 2016.
Mhe. Anne Semamba
Makinda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Ali Mchumo.Katika
hatua nyingine, Rais Magufuli amemteua Prof.
Apollinaria Elikana Pereka kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Teknolojia Dar
es salaam (Dar es salaam Institute of Technology - DIT).
Prof. Apollinaria
Elikana Pereka ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) Morogoro.Prof. Pereka
anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Prof. Fredrick Mwanuzi ambaye amemaliza
muda wake.
Uteuzi huu umeanza
leo tarehe 30 Mei, 2016.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano,
IKULU
Dar es salaam
30 Mei, 2016

0 comments:
Post a Comment