Na Anitha Jonas – MAELEZO.
“Wahenga
wanasema penye nia pana njia na haja ya mja hunena, muungwana ni
vitendo.” Hatimae Serikali imetimiza ndoto zake za kuwa na kituo bora
chenye kutoa taarifa za uhakika zinazohusu masuala ya hali ya hewa
katika kiwango cha Kimataifa.
Serikali
imeweza kufanikisha hili kwa kupitia taasisi yake ya Mamlaka ya Hali ya
Hewa (TMA) ambapo mpaka sasa imefanikiwa kuboresha huduma hizo kwa
asilimia 80. Haya ni mafanikio makubwa kutokana na ukweli kwamba
kufahamu habari za hali ya hewa kunasaidia sana kupanga shughuli za
kiuchumi na maendeleo.
Hilo
limejidhihirisha hivi karibuni katika taarifa ya tahadhari kuwepo kwa
mvua zitakazo ambatana na upepo kutokana na kuimarika kwa ukanda wa mvua
sambamba na uwepo wa kimbunga Fantala katika Bahari ya Hindi.
Taarifa
hiyo ilitolewa na Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Hali ya Hewa, Dkt. Agness
Kijazi na kusema mvua hizo zinatarajiwa kunyesha kuanzia Aprili
13-16,2016 ambapo kutakuwa na mvua kubwa inayozidi milimita 50 ndani ya
saa 24. na hili limetokea kama lilivyotabiriwa. Wenye kuchukua tahadhari
wamesha hivyo na kuepuka madhara yatokanayo na mafuriko. Waliohama
baadhi ya sehemu za mabondeni, walishukuru baada ya kuona makazi yao ya
awali yakifunikwa kabisa na maji.
Mvua hizo zilikuwa zikiathiri mkoa wa Tanga, Dar es Salaam, Pwani,Morogoro pamoja na visiwa vya unguja na Pemba.
Kuthibitisha
kuwa kituo hicho kinatoa taarifa za uhakika ni pale ambapo mwaka jana
Dkt. Agness Kijazi alitangaza kuwepo na mvua za EL-NINO kuanzia mwanzoni
mwa mwezi Septemba–Desemba 2015. Hii ilithibitika baada kushuhudia
kuwepo kwa mvua hizo katika maeneo mbali mbali ya nchi ambapo
mvua hizo zilisababisha mafuriko na uharibifu wa miundombinu,makazi na
mazao ya wakulima.
Utabiri huo wa kuaminika unatokana na TMA kuboresha mtandao wa vituo na usimikaji wa mitambo ya hali ya hewa pamoja na kuongeza idadi ya vituo vya hali ya hewa ambapo vituo vitatu vyenye mitambo ya kisasa vimejengwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo Kilwa Masoko- Lindi, Mpanda-Katavi na Songwe.Vituo hivi vimechangia kuongeza upatikanaji wa takwimu na taarifa za hali ya hewa kwa shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi nchini.
Kwa
sasaSerikali kupitia TMA imeanzisha kituo cha kupimia hali ya hewa na
Kilimo kiitwacho Agromet Station hukoMatangutuani Pemba na hivyo
kuongeza idadi ya vituo vya kutoa huduma za hali ya hewa katika sekta ya
Kilimo na kufikia vituo 15 nchini,hivyo kuongeza ubora wa taarifa
zinazotolewa.
Kwa
upande wa taarifa za anga ya juu Mamlaka imeimarisha huduma za Usafiri
wa Anga kwa kuboresha mtambo wa kupima hali ya hewa katika anga za juu
(Modernization of Upper Air System) katika kiwanja cha Ndege cha
Kimataifa cha Julius Nyerere Dar es Salaam (JNIA) pamoja na kufufua
kituo cha kupima taarifa za anga ya juu kilichopoTabora.
TMAkatika
kuimarisha huduma za utoaji wa taarifa za hali ya hewa nchini
imefanikiwa kuanzisha vituo 11 vya kupima hali ya hewa nchini katika
kipindi 2010-2015 ambapo vituo hivyo vimewekwa maeneo mbalimbali ikiwemo
Moshi(Kisangesangeni,Maweni,UparonaMasila,Lindi,Nachingwea,Tunduru,Msata
(Bagamoyo),Nzega (Tabora),Makete (Njombe) na Chanika (Dar es Salaam).
Ili kufikia viwango vya kimataifa kwa masuala ya upimaji wa hali ya hewaa Dkt.Kijazi anabainishakuwa Mamlaka imenunua Mitambo Mitano (5) ya Kisasa ya kupima hali ya hewa inayojiendesha yenyewe (Automatic Weather Station) kupitia mradi wa Mobile Weather Alert. Mitambo hiyo imekwishafungwa katika sehemu mbalimbali hapa nchini,pamoja na mtambo wa kuchambua data (Computer Cluster) ambao umefungwa katika JNIA na hivyo kusaidia kuboresha utabiri wa hali ya hewa hususani kwa watumiaji waZiwa Nyasa na Victoria.
“Kuna
Mitambo mingine 16 ya kupima hali ya hewa nchini ambayo imenunuliwa
kupitia mradi wa (CIRDA) chini ya udhamini wa Shirika la Maendeleo
(UNDP) ambapo taratibu za kufunga mitambo hiyo zimekamilika kwa asilimia
kubwa”aliongeza Dkt.Kijazi.
Mbali na hayo Mamlaka kwa sasa hutoa huduma za hali ya hewa katika Bandari ya Zanzibar pamoja na ZiwaVictoria, Ziwa Nyasa na Ziwa Tanganyika – Kigoma na kuboreshwa kwa huduma hizo katika maeneo hayo kumeifanya Mamlakakuweza kutoa utabiriwa hali ya hewa katika Maziwa yote nchini tofauti na ilivyokuwa awali kwamba utabiri wa hali ya hewa ulikuwa ukifanyika katika bahari tu.
Katika uboreshaji huu, Mamlaka imeanzisha vituo viwili vya Rada za hali ya hewa katika eneo la Bangulo,Dar es Salaam tangu Aprili 2011 pamoja na kituo cha Kiseke – Mwanza ambacho kimekamlika hivi karibuni. Vituo hivi vimekuwa mchango mkubwa katika kutoa taarifa za uhakika kwa wakati. Rada za hali ya hewa ni muhimu katika uboreshaji wa utabiri wa hali ya hewa hususani katika utabiriwa hali mbaya ya hewa.
Pamoja
na hayo Mamlaka inamiliki mtambo unaotumika kuhakiki vifaa vya kupimia
mkandamizo wa hewa (Pressure Calibration Unit) ambao umefungwa katika
karakana ya Mamlaka ya Hali ya hewa iliyopo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Julius Nyerere Dar es Salaam eneo la UwanjaMdogo (Terminal 1).
Aidha,Mamlaka ya Hali ya Hewa kwa kushirikiana na Idara ya Mazingira, Ofisi ya Makamu wa Rais pamoja na vyuo vikuu nchini inafanya tafiti mbalimbali za mabadiliko ya hali ya hewa kama vile Mradi wa Climate Change Impact Adaptation and Mitigation-(CCIAM) ambapo pia tafiti juu ya elimu ya asili ya utabiri wa hali ya hewa (Indigenous knowledge) zinafanyika.
Mbali
na hayoSerikali kupitia TMA imeboresha Chuo cha Hali ya Hewa Kigoma kwa
kuongeza idadi ya walimu, vitendea kazi na kuboresha miundombinu ya
Chuo na kuhakikisha kinapata usajili wa NACTE.Chuo hicho hutoa Mafunzo
ya Diploma katika fani ya hali ya hewa (Meteorological Technician Senior Level Course).
Hata
hivyo Mamlaka kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam imekuwa
ikitoa Shahada ya kwanza ya Sayansi ya Hali ya Hewa (BSc, Meteorology)
kuanzia mwaka wa masomo 2013/2014.
TMA kwa kushirikiana na Kampuni za simu za mkononi zaVodacom na Tigo imekuwa ikitoa tarifa za huduma za hali ya hewa kupitia ujumbe mfupi wa maandishi wa simu za mkononi (sms) na lengo likiwa ni kurahisisha upatikanaji wa tarifa za hali ya hewa kwa umma.
Mbali
na hayo naye Bi. Merry Kadaya mkazi wa Kilosa,Mkoa wa Morogoro
alipohojiwa kuhusu taarifa za hali ya hewa zinazotolewa na TMA alisema
anaipongeza Mamlaka kwa kazi wanayoifanya kwani kwa sasa wamekuwa
wananatoa taarifa za uhakika zisizona na shaka,pia ameiomba serikali
kujiandaa pale wanapopata taarifa hizo ili kuwaweza kuwaokoa wananchi.
Halikadhalika,takwimu
za hali ya hewa zina umuhimu katika shughuli mbalimbali kama katika
tafiti za Mafuta na Gesi (Oil and gas exploration) pamoja naMipango ya
Maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii. Mkulima anategemea sana kujua hali ya
hewa ili kilimo chake kiwe na tija. Utabiri wa hali ya hewa ni wa muhimu
sana pia kwenye suala zima la usafiri, ujenzi wa miundombinu kama
barabara, reli, viwanja vya ndege na madaraja. Hivyo uboreshaji na
ongezeko la vituo vya kisasa vya hali ya hewa ni hatua moja kubwa katika
maendeleo ya Taifa.
0 comments:
Post a Comment