Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » Serikali yaombwa kusaidia uingizwaji wa mafuta ya watu wenye ualbino

Serikali yaombwa kusaidia uingizwaji wa mafuta ya watu wenye ualbino

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na: Lilian Lundo – MAELEZO


Taasisi ya Josephat Torner Foundation inayojishughulisha na watu walemavu wameiomba Serikali kusaidia uingizaji wa mafuta ya ngozi kwa watu wenye albino nchini.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo Josephat Torner alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam ambapo alibainisha changamoto mbalimbali zinazo wakabili watu wenye ualbino.

“Watu wengi wenye ualbino wanaishi chini ya miaka 40 kutokana na kukosa mafuta ya kulinda ngozi dhidi ya miale ya jua, mafuta hayo huwasaidia kutoathilika na magonjwa ikiwemo kansa ya ngozi,” alisema Torner.

Torner alisema kuwa mafuta ya ngozi kwa watu wenye ualbino yanauzwa kati ya shilingi 30,000 na 40,000 kwa chupa ambapo mtu mwenye ualbino mmoja anatumia wastani wa chupa tano kwa mwaka.

Mkurugenzi huyo alisema kuwa gharama ya mafuta hayo ni kubwa kwa watu wenye ualbino ambao wengi wao wanaishi maisha ya chini na hasa wale wanaoishi vijijini ambao hawawezi kumudu kuyapata na kununua mafuta hayo.

Aidha, aliongeza kuwa kama Serikali itasaidia uingizwaji wa mafuta hayo na kupunguza ushuru ili yaingie nchini kama madawa kupitia Bohari Kuu ya Dawa (MSD) tofauti na hali ilivyo sasa ambapo yanatozwa kodi kama vipodozi, hatua hiyo itasaidia kupunguza kwa kiasi kubwa kushuka bei mafuta hayo na kuwafikia walengwa.

Kwa upande wake, Mratibu wa taasisi ya Afrikan Albino Foundation kutoka Netherland nchini Tanzania Bas Kreukniet amesema kuwa ikiwa Serikali itashiriki katika uingizaji wa mafuta hayo kuna uwezekano wa mafuta hayo kuuzwa shilingi 4,000 kwa chupa.

Aliongezea kuwa ikiwa bei ya mafuta hayo itapungua itawasaidia watu wengi wenye ualbino hasa wa kipato cha chini na wale waishio vijijini kutumia mafuta hayo na kuwasaidia kujikinga na miale ya jua.

Hadi sasa taasisi ya Afrikan Albino Foundation imeweza kuwasaidia watu wenye ualbino wapatao 13,000 tangu waanze kuleta mafuta hayo nchini mwaka 2004 ambapo kila mwezi jumla ya chupa 5,200 huingizwa nchini kwa ajili ya kuwasaidia watu wenye ualbino.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa