Na Raymond Mushumbusi WHSUM.
Serikali
imewapa miezi miwili wananchi waishio katika kijiji cha michezo cha
Changamani kilichopo Wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam kuhama katika eneo hilo kupisha uendelezwaji wa kijiji cha mchezo.
Agizo
hilo limetolewa na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Michezo kutoka Wizara ya
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bw. Alex Nkenyenge alipokutana na
wananchi hao katika kikao cha kujadili na kukubaliana muda wa kuhama
katika eneo hilo leo Jijini Dar es Salaam.
“Ndugu
zangu tumejadiliana wote na kukubaliana kuwa baada ya miezi miwili
mtakuwa mmeshaama katika eneo hilo kupisha uendelezwaji wa kijiji cha
michezo kwa ajili ya shughuli za mbalimbali za michezo” alisisitiza Bw.
Nkenyenge.
Naye
Kaimu Meneja wa Uwanja wa Taifa Bw.Julius Mgaya amesema kuwa mpango wa
kuwahamisha wananchi hao unalenga kutekeleza mradi wa kijiji cha michezo
kitakachojengwa kwa ajili ya kukuza na kuendeleza vipaji vya michezo
mbalimbali.
Kwa
upande wake mmoja ya wawakilishi wa wananchi hao Bw.Atillio Mballa
amesema wamekubaliana na muda huo waliopewa na watafikisha ujumbe huo
kwa wenzao na kabla ya muda hujafika watakuwa wameshatekeleza agizo
hilo.
Katika
mpango wa kukuza na kuendeleza michezo nchini Serikali imejipanga
kukuza sekta ya michezo nchini na kuifanya kuwa moja ya rasilimali
itakayochangia katika pato la taifa.

0 comments:
Post a Comment