Na:
Immaculate Makilika
Tanzania na China
kuendelea kuimarisha mahusiano katika nyanja mbalimbali zikiwemo za siasa,
uchumi na utamaduni.
Ziara ya hivi karibuni
ya kikazi ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikinao wa Afrika Mashariki, Dkt. Aziz
Mlima ,ikiwa ni mwaliko wa Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo ina lengo la kuimarisha mahusiano kati ya Tanzania na China
katika nyanja mbalimbali.
Katika ziara hiyo Dkt.
Mlima pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje
wa China Bw. Zhang Ming walifanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa
Serikali na wa makampuni makubwa ya China ambayo baadhi yameshawekeza nchini na mengine yameonesha dhamira ya kuwekeza.
Aidha, Serikali ya
China imesisitiza dhamira yake ya kukuza ushirikiano na Tanzania katika nyanja
ya uchumi kupitia uwekezaji kwenye sekta ya viwanda, nishati na miundombinu.
Huku kipaumbele kikiwa ni ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo, pamoja na maboresho ya
reli ya TAZARA na iko tayari kuanza upembuzi yakinifu wa Reli ya kati.
Kwa upande wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo,
kampuni ya China ya Merchant holding
International (CMHI), ambayo imeingia ubia na Serikali ya Tanzania na
Mfuko wa Oman kujenga bandari
hiyo kwa awamu ya kwanza ambayo itakamilika mwaka huu.
Vilevile, Serikali ya
China imebainisha kuwa imeshatenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu
wezeshe kama barabara, nishati ya umeme, maji, na TEHAMA.
Kuhusu reli ya TAZARA Serikali ya China imesema imeridhishwa na ityahanyia
kazi mazungumzo ya wataalamu yaliyofanyika jijini Dar es salaam hivi karibuni na
kuahidi kuendelea kuipa kipaumbele reli hiyo kwa kuwa inabeba
historia ya ya mahusiano yake na Afrika, na kutoa fedha kupitia itifaki ya 16
kwa ajili ya maboresho makubwa ya miundombinu ya reli hiyo, ikiwa ni pamoja na
kushiriki kikamilifu kwenye mikutano itakayofuata inayolenga namna bora ya
kuendesha reli hiyo kwa ushirikiano wa Tanzania na Zambia.

0 comments:
Post a Comment