Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Jacquiline Mrisho MAELEZO
Mamlaka
ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa mafunzo ya matumizi ya huduma za
mawasiliano kwa watumishi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo ili kupata muongozo utakaowasaidia kuepuka matumizi mabaya ya
mitandao ya kijamii.
Akifungua mafunzo hayo ya siku moja yaliyofanyika leo Jijini Dar es salaam, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Nuru Mllao amewataka watumishi wa wizara hiyo kuzingatia mafunzo hayo ili kuepuka matatizo ya mitandao ya kijamii wakati wakuteleza majukumu yao.
"Tumegundua
kwamba watumishi wanahitaji muongozo juu ya matumizi sahihi ya mitandao
ya kijamii, hivyo tunashkuru sana uongozi wa TCRA kukubali kutoa
mafunzo kwa watumishi wetu"alisema Bi.Nuru.
Aidha Bi Nuru ametoa rai kwa TCRA kutoa mafunzo hayo kwa watumishi wa wizara nyingine kwa kuwa watumishi wote wanatakiwa kupata miongozo juu ya matumizi sahihi na usalama wa huduma hizo.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Mhandisi James Kilaba, alisema kuwa matumizi ya mitandao ya kijamii yameongezeka hivyo kuchangia kuongezeka kwa changamoto za matumizi mabaya ya mitandao hiyo.
Kwa
upande wa huduma za mawasiliano ya simu, Mhandisi Kilaba alisema kuwa
mawasiliano ya simu yanakua kwa kasi nchini hali ambayo inaongeza
matumizi mabaya ya mawasiliano ya simu.
"Idadi
ya laini za simu kwa miaka 12 iliyopita ilikuwa ni milioni 2.3 lakini
hadi kufikia mwezi Machi mwaka huu idadi ya laini ni takribani milioni
40, wananchi ni wengi wanaotumia huduma za mitandao na wengi wao
wanaitumia vibaya”alisema Muhandisi Kilaba.
Mhandisi
Kilaba alielezea kuwa mafunzo hayo yataegemea kwenye nyanja za kukua
kwa sekta ya mawasiliano na changamoto zake pamoja na mambo muhimu ya
kuzingatia katika matumizi ya mitandao ya kijamii.
Alisisitiza kuwa kupitia mafunzo hayo watumishi wataweza kujua matumizi sahihi ya mitandao hasa katika shughuli zao za kiofisi.
Katika
kuzingatia usalama wa mawasiliano yao, TCRA imewashauri watumishi
pamoja na wananchi kwa ujumla kutotumia nywila (password) moja kujiunga
kwenye mtandao zaidi ya mmoja.
Aliwataka
kutoweka nywila ambazo zinahusisha mambo binafsi ambayo yanajulikana
kwa watu wengi ili kuzuia mtu mwingine asipate urahisi wa kubuni kuingia
katika mtandao wa mtu mwingine.
0 comments:
Post a Comment