Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mtaalam Mshauri wa Master Card Foundation Gabriel Kivuti akifafanua jambo katika
semina ya namna shirika hilo linavyofanya kazi na jinsi ya kushiriki
shindano la mwaka 2016 ili kupata washindi watakaopata msaada wa kifedha
na kuboresha ushirikishwaji wa kifedha kwa wakulima wadogo Afrika.
Mtaalam Mshauri wa Master Card Foundation Gabriel Kivuti akieleza jambo kwa waandishi
wa habari juu ya kushiriki shindano la kuongeza kipato lijulikanalo
kama “Scaling Competition” kwa makundi yanayoruhusiwa kushiriki shindano
hilo kuwa ni pamoja na vikundi vya akiba, bima ndogo ndogo na mifumo ya
umoja wa fedha, fomu za maombi na mwongozo wa kushiriki shindano hilo
zinapatikana katika tovuti ya www.frp.org .
Na: Lilian Lundo - Maelezo
Watanzania wameombwa kujitokeza kwa wingi kushiriki shindano la kuongeza kipato lijulikanalo kama “Scaling Competition” kwa kutuma maombi yao shirika
la “Master Card Foundation, Fund For Rural Prosperity” ili kupanua na
kuimarisha upatikanaji wa fedha Vijijini Tanzania.
Hayo
yalisemwa na Mtaalam Mshauri wa Master Card Foundation Gabriel Kivuti
leo, jijini Dar es Salaam katika semina ya namna shirika hilo
linavyofanya kazi na jinsi ya kushiriki shindano la mwaka 2016 ili
kupata washindi watakaopata msaada wa kifedha na kuboresha
ushirikishwaji wa kifedha kwa wakulima wadogo Afrika.
“Master Card Foundation inafanya kazi na mashirika yenye maono ili kuleta zaidi upatikanaji wa
elimu, mafunzo ya ujuzi na huduma za kifedha kwa watu wanaoishi katika
umaskini barani Afrika, ikiongozwa na dira ya kuboresha mafunzo na
kuongeza ushirikishwaji wa upatikanaji wa kifedha ili kupunguza
umaskini,” alisema Kivuti.
Kivuti alisema kuwa, kaya nyingi za
vijijini barani Afrika hazishirikishwi katika masuala ya kifedha na
zaidi ya asilimia 70 za familia Kusini mwa Jangwa la Sahara sehemu kubwa
ya mapato yao yanatokana na shughuli za kilimo, wakati huohuo watoa
huduma za kifedha wanakabiliana na changamoto kadhaa katika kuifikia jamii, hivyo Master Card likaamua kusaidia miradi ambayo ina uwezo wa kuleta mabadiliko chanya.
Aidha,
Kivuti alitaja makundi yanayoruhusiwa kushiriki shindano hilo kuwa ni
pamoja na vikundi vya akiba, bima ndogo ndogo na mifumo ya umoja wa
fedha, fomu za maombi na mwongozo wa kushiriki shindano hilo
zinapatikana katika tovuti ya www.frp.org .
Jumla
ya dola za Kimarekani milioni 10.6 zimetolewa kwa washindi wa mwaka
2015 kwa ajili ya maendeleo Vijijini, kampuni zilizoshinda ni APA Insurance Ltd kutoka Kenya, Finserve Afrika Ltd/Equitel kutoka Uganda, M-KOPA LLC kutoka Tanzania, Musoni
Kenya Ltd kutoka Kenya na Olam Uganda Ltd kutoka Uganda. Kupitia
kampuni hizo takribani watu milioni nane wanaoishi maeneo ya Vijijini
watakuwa na fursa ya kupata huduma za kifedha ifikapo mwaka 2020.
( PICHA NA BEATRICE LYIMO- MAELEZO)
0 comments:
Post a Comment