Na Benedict Liwenga-MAELEZO.
Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imepokea msaada wa
vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi bilioni 1.4 ikiwa ni sehemu ya
mkakati wa kutoa chanjo kwa akina mama na watoto dhidi ya magonjwa
mbalimbali nchini.
Akiongea na waandishi wa habari Wizarani hapo, Mkurugenzi wa Huduma za Kinga, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Neema Rusibimayila ameeleza kuwa vifaa tiba hivyo vitasaidia uhifadhi
wa chanjo katika mikoa mbalimbali pamoja halmashauri nchini.
‘’Ni
msaada mkubwa tulioupata toka WHO na nina amini kuwa utatusaidia sana
katika kufanikisha suala la chanjo kwa akina mama na watoto nchini na
pia tunaamini wataendela kushirikiana na Wizara ili tuweze kufikia
malengo tuliyojiwekea’’, alisema Dkt. Rusibimayila.
Ameongeza
kuwa, kwa sasa vituo vipya vinavyofunguliwa nchini vikiwemo vile
ambavyo havikuwa na majokofu vitakuwa na uwezo wa kupata vifaa hivyo
kama vile majokofu na vifaa vingine vya tiba ili huduma za chanjo ziweze
kutolewa katika kila kituo nchini.
Akikabidhi vifaa hivyo Wizarani hapo, Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Tanzania Dkt. Rufaro Chatoro amesema
kuwa vifaa hivyo vyenye thamani ya shilingi bilioni 1.4 ni pamoja na
majokofu 200 pamoja na vifaa vitumikavyo kwa ajili ya kutolea chanjo.
Kwa
upande wake Mratibu Chanjo Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Bwana Emmanuel Yohana ameeleza kuwa, majokofu hayo pia
yatapelekewa katika wilaya ambayo yana upungufu wa majokofu pamoja na
vituo vipya kwa ajili ya kupunguza umbali kwa wagonjwa wa chanjo na pia
ni moja ya kuweka huduma karibu na wananchi nchini.
Aidha,
ameongeza kuwa spesimeni za polio na surua zilizotolewa na WHO
zitapalekwa pia katika vituo kwa jili ya kuchukua damu kwa ajili ya
vipimo na kuletwa Dar es Salaam kwa uchunguzi zaidi wa maabara.
‘’Wanufaika
wa huu msaada kutoka WHO ni wananchi wote wa Tanzania kwani utaenda
katika vituo vyote vya chini zikiwemo Zahanati’’, alisema Yohana.
Kupitia
wadau mbalimbali Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto inaendelea kushirikiana na wadau hao katika kutafuta vifaa tiba
mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha kuwa sekta ya afya nchini inaimarika
kwani Tanzania kwa sasa imeweza kudhibiti polio kwa kiasi kikubwa.
0 comments:
Post a Comment