Home » » MBWANA SAMATTA PAMOJA NA WASANII WA SHIWATA WAKABIDHIWA MAENEO YAO KATIKA KIJIJI CHA WASANII WILAYANI MKURANGA.

MBWANA SAMATTA PAMOJA NA WASANII WA SHIWATA WAKABIDHIWA MAENEO YAO KATIKA KIJIJI CHA WASANII WILAYANI MKURANGA.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sanaa wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Leah Kihimbi (kushoto) akisalimiana na Afisa Utamaduni Mstaafu wa Wizara hiyo Bw. Michael Kagondela pamoja na Mwenyekiti wa Shirikisho la Wasanii Tanzania (SHIWATA) Bw. Casim Taalib (katikati) mara alipowasili katika kijiji cha Mwanzega Wilayani Mkuranga kwa aajili ya hafla ya kuwagawia maeneo Wasaanii pamoja na Mwanasoka bora ndani ya Afrika Bw. Mbwana Samatta 5 Juni, 2016.

Afisa Utamaduni Wilaya ya Mkuranga, Bw. Pembe Mlekwa (kushoto) akiwa ameongozana na na wadau mbalimbali wa masuala ya sanaa na michezo pamoja na mjumbe toka Halmashauri Wilayani hapo kuelekea katika eneo la ugawaji maeneo kwa wasanii na Mwanasoka bora ndani ya Afrika, Bw. Mbwana Samatta 5 Juni, 2016.

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sanaa wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Leah Kihimbi (kushoto) akizungumza na Afisa Utamaduni Mstaafu wa Wizara hiyo Bw. Michael Kagondela pamoja na Mwenyekiti wa Shirikisho la Wasanii Tanzania (SHIWATA) Bw. Casim Taalib (katikati) mara alipowasili katika kijiji cha Mwanzega Wilayani Mkuranga kwa aajili ya hafla ya kuwagawia maeneo Wasaanii pamoja na Mwanasoka bora ndani ya Afrika Bw. Mbwana Samatta 5 Juni, 2016.

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sanaa wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Leah Kihimbi (wa pili kushoto) akiwa ameongozana na Mwenyekiti wa Shirikisho la Wasanii Tanzania (SHIWATA) Bw. Casim Taalib (kushoto) pamoja na Afisa Utamaduni Wilaya ya Mkuranga, Bw. Pembe Mlekwa (wa pili kulia) mara alipowasili katika kijiji cha Mwanzega Wilayani Mkuranga kwa aajili ya hafla ya kuwagawia maeneo Wasaanii pamoja na Mwanasoka bora ndani ya Afrika Bw. Mbwana Samatta 5 Juni, 2016.

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sanaa wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Leah Kihimbi(wa pili kulia) akisalimiana na baadhi ya Viongozi wa Kijiji Wilayani Mkuranga mara alipowasili katika kijiji cha Mwanzega Wilayani Mkuranga kwa aajili ya hafla ya kuwagawia maeneo Wasaanii pamoja na Mwanasoka bora ndani ya Afrika Bw. Mbwana Samatta 5 Juni, 2016 Wilayani Mkuranga.

Baadhi ya Wasanii pamoja na Wanakijiji wakiwa wamesimama kumpokea mgeni rasmi ambaye ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sanaa wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Leah Kihimbini ambaye alimwakilisha Waziri Nape Nnauye katika hafla ya uwagawaji maeneo kwa ajili ya wasanii na Mwanasoka bora wa ndani ya Afrika, Bw. Mbwana Samatta 5 Juni, 2016 Wilayani Mkuranga.

Kikundi cha matarumbeta toka Wilayani Mkuranga kikitumbuiza wakati wa hafla ya uwagawaji maeneo kwa ajili ya wasanii na Mwanasoka bora wa ndani ya Afrika, Bw. Mbwana Samatta 5 Juni, 2016 Wilayani Mkuranga.

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sanaa wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Leah Kihimbi (katikati) akiteta jambo na Mwenyekiti wa Shirikisho la Wasanii Tanzania (SHIWATA) Bw. Casim Taalib (kushoto) wakati wa hafla ya uwagawaji maeneo kwa ajili ya wasanii na Mwanasoka bora wa ndani ya Afrika, Bw. Mbwana Samatta 5 Juni, 2016 Wilayani Mkuranga. Kulia ni Afisa Utamaduni Wilayani Mkuranga, Bw. Pembe Mlekwa.


Jiwe la Msingi linaloashiria ujenzi wa Kijiji cha Wasanii Wilayani Mkuranga lililowekwa wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2014 Wilayani Mkuranga.


Baadhi ya Wasanii pamoja na Wanakijiji wakifuatilia hafla ya uwagawaji maeneo kwa ajili ya wasanii na Mwanasoka bora wa ndani ya Afrika, Bw. Mbwana Samatta 5 Juni, 2016 Wilayani Mkuranga.

Afisa Utamaduni Mstaafu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Michael Kagondela (kushoto) akijadiliana na Afisa Utamaduni mwenzie toka Wilaya ya Mkuranga, Bw. Pembe Mlekwa kabla ya kuanza kwa hafla ya uwagawaji maeneo kwa ajili ya wasanii na Mwanasoka bora wa ndani ya Afrika, Bw. Mbwana Samatta 5 Juni, 2016 Wilayani Mkuranga.

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sanaa wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Leah Kihimbi(kulia) akiwa amekaa meza kuu pamoja na familia ya mzee Mbwana Samatta (wa pili kushoto) aliyeambatana na mkewe. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Shirikisho la Wasanii Tanzania (SHIWATA) Bw. Casim Taalib tayari kwa kuanza hafla ya uwagawaji maeneo kwa ajili ya wasanii na Mwanasoka bora wa ndani ya Afrika, Bw. Mbwana Samatta 5 Juni, 2016 Wilayani Mkuranga.



Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sanaa wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Leah Kihimbi akiwahutubia baadhi ya Wasanii na Wanakijiji waliohudhuria hafla ya uwagawaji maeneo kwa ajili ya wasanii na Mwanasoka bora wa ndani ya Afrika, Bw. Mbwana Samatta 5 Juni, 2016 Wilayani Mkuranga.



Mwenyekiti wa Shirikisho la Wasanii Tanzania (SHIWATA) Bw. Casim Taalib (aliyesimama) akiongea na baaadhi ya Wasanii pamoja na Wanakijiji waliohudhuria hafla ya uwagawaji maeneo kwa ajili ya wasanii na Mwanasoka bora wa ndani ya Afrika, Bw. Mbwana Samatta 5 Juni, 2016 Wilayani Mkuranga.

Baadhi ya Wasanii pamoja na Wanakijiji wakimsikiliza  Mwenyekiti wa Shirikisho la Wasanii Tanzania (SHIWATA) Bw. Casim Taalib (hayupo pichani) wakati wa hafla ya uwagawaji maeneo kwa ajili ya wasanii na Mwanasoka bora wa ndani ya Afrika, Bw. Mbwana Samatta 5 Juni, 2016 Wilayani Mkuranga.


Afisa Utamaduni Mstaafu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Michael Kagondela (kulia) akiwataja kwa majina baadhi ya wasanii waliogawiwa maeneo yao
wakati wa hafla ya uwagawaji maeneo kwa ajili ya wasanii na Mwanasoka bora wa ndani ya Afrika, Bw. Mbwana Samatta 5 Juni, 2016 Wilayani Mkuranga.

Baadhi ya Wasanii wakiwa wamejipanga mstari mara baada ya kuitwa majina na Afisa Utamaduni Afisa Utamaduni Mstaafu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Michael Kagondel (hayupo pichani) tayari kwa kupewa maeneo yao waliochangia katika Shirikisho lao 5 Juni, 2016 Wilayani Mkuranga.

Mzee Mbwana Samatta akiishukuru Serikali kwa msaada aliopewa mwanae Mbwana Samatta kwa kupewa eneo la ukubwa wa ekari tano 5 Juni, 2016 Wilayani Mkuranga.

Msanii wa masuala ya Abstract Painting, Bw. Faridu Mathias Taratib akiishukuru Serikali kwa niaba ya Wasanii wenzie kwa kupewa maeneo ya kuendeleza kijiji cha Wasanii 5 Juni, 2016 Wilayani Mkuranga.

Mdau kutoka Mfuko wa Pensheni PSPF akiwahamasisha Wasanii kujiunga na huduma zitolewazo na Mfuko huo wakati wa hafla ya uwagawaji maeneo kwa ajili ya wasanii na Mwanasoka bora wa ndani ya Afrika, Bw. Mbwana Samatta 5 Juni, 2016 Wilayani Mkuranga.

Afisa Utamaduni Wilayani Mkuranga, Bw. Pembe Mlekwa (kulia) akiongea na baadhi ya Wasanii na Wanakijiji waliohudhuria hafla ya uwagawaji maeneo kwa ajili ya wasanii na Mwanasoka bora wa ndani ya Afrika, Bw. Mbwana Samatta 5 Juni, 2016 Wilayani Mkuranga.



Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sanaa wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Leah Kihimbi (kulia) akimpongeza mama yake Mbwana Samatta wakati wa hafla ya uwagawaji maeneo kwa ajili ya wasanii na Mwanasoka bora wa ndani ya Afrika, Bw. Mbwana Samatta 5 Juni, 2016 Wilayani Mkuranga.

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sanaa wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Leah Kihimbi (kulia) akimpongeza Kaka yake Mbwana Samatta, Bw. Mohamed Samatta wakati wa hafla ya uwagawaji maeneo kwa ajili ya wasanii na Mwanasoka bora wa ndani ya Afrika, Bw. Mbwana Samatta 5 Juni, 2016 Wilayani Mkuranga.

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sanaa wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Leah Kihimbi (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na familia ya Mzee Mbwana Samatta, baadhi ya Viongozi Wilayani Mkuranga pamoja na Wadau wengine wakati wa hafla ya uwagawaji maeneo kwa ajili ya wasanii na Mwanasoka bora wa ndani ya Afrika, Bw. Mbwana Samatta 5 Juni, 2016 Wilayani Mkuranga.

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sanaa wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Leah Kihimbi (kulia) akimkabidhi cheti kaka yake Mbwana Samatta kwa niaba yake wakati wa hafla ya uwagawaji maeneo kwa ajili ya wasanii na Mwanasoka bora wa ndani ya Afrika, Bw. Mbwana Samatta 5 Juni, 2016 Wilayani Mkuranga.

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sanaa wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Leah Kihimbi (kulia) akimkabidhi cheti mmoja ya Wasanii wakati wa hafla ya uwagawaji maeneo kwa ajili ya wasanii na Mwanasoka bora wa ndani ya Afrika, Bw. Mbwana Samatta 5 Juni, 2016 Wilayani Mkuranga.  
Mwenyekiti wa Shirikisho la Wasaanii Tanzania (SHIWATA) Bw. Casim Taalib (wa pili kushoto) akimpa maelezo Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sanaa wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Leah Kihimbi (katikati)  wakati wa ukgauzi wa nyumba zilizogawiwa kwa ajili ya Wasanii na Mwanasoka bora wa ndani ya Afrika, Bw. Mbwana Samatta 5 Juni, 2016 Wilayani Mkuranga. kuhusiana na nyumba za Wasanii

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sanaa wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Leah Kihimbi (wa pili kulia) akiwa ameongozana na Mwenyekiti wa Shirikisho la Wasaanii Tanzania (SHIWATA) Bw. Casim Taalib (kulia) pamoja na Afisa Utamaduni Wilayani Mkuranga kukagua nyumba za Wasanii 5 Juni, 2016 Wilayani Mkuranga.


Baadhi ya nyumba katika kijiji cha Wasaanii kama zinavyoonekana katika picha Wilayani Mkuranga.

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sanaa wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Leah Kihimbi (katikati) akimkabidhi cheti cha umiliki wa eneo la ukubwa wa ekari tano baba yake Mbwana Samatta kwa niaba ya mwanae Mbwana Samatta wakati wa hafla ya uwagawaji maeneo kwa ajili ya wasanii na Mwanasoka huyo bora wa ndani ya Afrika Juni, 2016 Wilayani Mkuranga.

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sanaa wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Leah Kihimbi (kulia) akimkabidhi cheti cha umiliki wa nyumba, Msanii wa masuala ya Abstract Painting, Bw. Faridu Mathias Taratib wakati wa hafla ya uwagawaji maeneo kwa ajili ya wasanii na Mwanasoka bora wa ndani ya Afrika, Bw. Mbwana Samatta 5 Juni, 2016 Wilayani Mkuranga.
(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA, MAELEZO)

NA BENEDICT LIWENGA, MAELEZO.


WASANII nchini wamehimizwa kuchangamkia fursa ya kujiunga na Shirikisho la Wasanii Tanzania (SHIWATA) ambao ndiyo waanzilishi wa kijiji maalum cha wasanii kilichopo Wilayani Mkuranga, lengo likiwa kuwavutia wasanii hao kuhamia katika kijiji hicho.

Kauli hiyo imetolewa jana na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sanaa, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Leah Kihimbi wakati wa hafla maalum ya kuwakabidhi maeneo wasanii 35 akiwemo Mwanasoka Mahiri wa Tanzania anayechezea soka la Kulipwa nchini Ubelgiji Bw. Mbwana Samata.

Bi. Kihimbi amewapongeza baadhi ya wasanii wa Shirikisho hilo kwa uthubutu wao wa kujiunga ndani ya kijiji hicho na kupata nafasi ya kujengewa makazi yao.

Katika hafla hiyo, wasanii mbalimbali nchini wamefanikiwa kupewa vyeti vya umiliki wa maeneo yao waliyogawiwa kulingana na pesa za michango yao katika Shirikisho lao huku akiwataka wasanii wengine kuiga mfano huo.

"Nimeambiwa kuwa Shirikisho hili la SHIWATA linafanya kazi zake kwa kuwashirikisha wadau wake kama vile kufanya warsha, makongamano, mafunzo ya kitaaluma na ujasiriamali, kwahiyo naamini kijiji hiki kitasheheni sifa zote hizi", alisema Kihimbi.

Akizungumzia suala la miradi miwili katika eneo hilo, alisema kuwa SHIWATA imechagua eneo zuri huku akiahidi kuzifikisha kwa Waziri mwenye dhamana katika Wizara yake, Mhe. Nape Nnauye baadhi ya changamoto zilizopo ndani ya eneo hilo kama vile barabara, maji pamoja na umeme ili wasanii wasipatwe na sumbufu wowote pindi wanapohamia kijijini hapo.

"Nimeambiwa kuwa huku kuna Miradi miwili ya ekari 500 katika kijiji cha Ngarambe ambayo ni mashamba makubwa pamoja na ekari 300 ambazo ndo hizi tulizopo hapa, naipongeza Halmashauri ya Mkuranga kwa jambo hili zuri na kwakweli SHIWATA katika hili hawajafanya makosa kuchagua eneo hili, niwaahidi kuwa nitazifikisha baadhi ya changamoto mlizoniambia katika eneo hili kwa Mhe. Waziri kwani yeye anapenda sana kuona maendeleo katika tasnia hii", alisema Kihimbi.

Kwa upande wake Afisa Utamaduni Wilaya ya Mkuranga Bw. Pembe Mlekwa alieleza kuwa, Wilaya yake imekuwa ikifanya jitihada za kuwawezesha wasanii kupatiwa maeneo hayo wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2014 lengo likiwa kuitambulisha Tanzania na Dunia kwa ujumla.

"Lengo la Wilaya yetu la kutenga maeneo haya ni kuitambulisha Tanzania na Dunia kwa ujumla kuwa kuna kijiji cha Wasanii hapa nchini, kama ilivyo kule kwa wenzetu kama vile Hollywood nchini Marekani, ili wasanii wetu nao wajisikie kuwa wana eneo lao maalum", alisema Mlekwa.

Naye baba wa Mwanasoka bora wa Tanzania Mzee Mbwana Samatta ameipongeza Serikali kwa kumpatia mwanae eneo lenye ukubwa wa ekari tano ambapo mwanasoka huyo ameahidi kujenga Kituo cha Michezo cha Vijana (Sports Academy) ili vijana ndani na nje ya nchi waweze kuja na kupatiwa ujuzi na kupafanya mahali hapo kujulikana kote ulimwenguni.

"Mbwana Samatta ameniambia kuwa anataka kupafanya mahali hapa kuwa mahali pa Kimataifa kwani anataka kuanzisha Kituo Maalum cha Wanasoka kuja kujifua hasa vijana wadogo toka ndani na nje ya Tanzania", alisema mzee Samatta.

Katika hafla hiyo, jumla ya wasanii 35 wamepatiwa vyeti vya umiliki wa maeneo yao pamoja na ekari tano zimetolewa kwa ajili ya kumzawadia Mbwana Samatta kwa kuifanyia Tanzania kung'ara katika soka ulimwenguni.



 

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa