Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
NA BENEDICT LIWENGA, MAELEZO.
Wasanii nchini wamehimizwa kuchangamkia fursa ya kujiunga na Shirikisho
la Wasanii Tanzania (SHIWATA) ambao ndiyo waanzilishi wa kijiji maalum
cha wasanii kilichopo Wilayani Mkuranga, lengo likiwa kuwavutia wasanii
hao kuhamia katika kijiji hicho.
Kauli hiyo
imetolewa leo na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sanaa, Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Leah Kihimbi wakati wa hafla maalum ya
kuwakabidhi maeneo wasanii 35 akiwemo Mwanasoka Mahiri wa Tanzania
anayechezea soka la Kulipwa nchini Ubelgiji Bw. Mbwana Samata.
Bi. Kihimbi
amewapongeza baadhi ya wasanii wa Shirikisho hilo kwa uthubutu wao wa
kujiunga ndani ya kijiji hicho kwa kupata nafasi ya kujengewa makazi
yao.
Katika hafla hiyo, wasanii mbalimbali nchini wamefanikiwa kupewa vyeti vya umiliki wa maeneo waliyogawiwa kulingana na pesa za michango yao huku akiwataka wasanii wengine kuiga mfano huo.
"Nimeambiwa
kuwa Shirikisho hili la Shiwata linafanya kazi kwa kuwashirikisha wadau
wake kama vile warsha,makongamano, mafunzo ya kitaaluma na ujasiriamali
kwahiyo naamini kijiji hiki kitasheheni sifa zote hizi", alisema
Kihimbi.
Akizungumzia
suala la miradi miwili katika eneo hilo, amesema kuwa Shiwata imechagua
eneo zuri huku akiahidi kuzifikisha kwa Waziri mwenye dhamana, Mhe. Nape
Nnauye baadhi ya changamoto zilizopo ndani ya eneo hilo kama vile
barabara, maji pamoja na umeme.
" Nimeambiwa
kuwa kuna miradi hii miwili ya ekari 500 katika kijiji cha Ngarambe
ambayo ni mashamba makubwa na ekari 300 ambazo ndo hizi tulizopo,
naipongeza Halmashauri ya Mkuranga kwa jambo hili zuri na Shiwata
hawajafanya makosa kuchagua eneo hili, naahidi kuzifikisha baadhi ya
changamoto za hapa kwa Mhe. Waziri kwani yeye anapenda sana kuona
maendeleo katika tasnia hii", alisema Kihimbi.
Kwa upande
wake Afisa Utamaduni Wilaya ya Mkuranga Bw. Pembe Mlekwa ameeleza kuwa,
Wilaya yake imekuwa ikifanya jitihada za kuwawezesha wasanii kupatiwa
maeneo wakati wa mbio za mwenge mwaka 2014 lengo likiwa kuitambulisha
Tanzania na Dunia kwa ujumla.
"Lengo la
Wilaya yetu la kuweka maeneo haya ni kuitambulisha Tanzania na Dunia kwa
ujumla kuwa kuna kijiji cha Wasanii hapa nchini, kama ilivyo kule kwa
wenzetu kama vile Hollywood nchini Marekani, ili wasanii wetu nao
wajiskie kuwa wana eneo lao", alisema Mlekwa.
Naye baba wa
Mwanasoka bora wa Tanzania Mbwana Samata ameipongeza Serikali kwa
kumpatia mwanae eneo lenye ukubwa wa ekari tano ambapo mwanasoka huyo
ameahidi kujenga Kituo cha Mafunzo cha Michezo ili vijana ndani na nje
ya nchi waweze kuja na kupatiwa ujuzi.
" Mbwana
Samata ameniambia kuwa anataka kupafanya mahali hapa kuwa pa Kimataifa
kwani anataka kuanzisha Kituo Maalum cha Wanasoka kuja kujifua hasa
vijana wadogo toka ndani na nje ya Tanzania", alisema mzee Samata.
Katika hafla
hiyo, jumlanya Wasanii 35 wamepatiwa vyeti vya umiliki wa maeneo yao
pamoja na ekari tano zimetolewa kwa ajili ya kumzawadia Mbwana Samata
kwa kuifanyia Tanzania kung'ara katika soka.
0 comments:
Post a Comment