Home » » MeTL yang’ara tuzo za Rais

MeTL yang’ara tuzo za Rais

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Mohammed Dewji.
KAMPUNI tanzu ya MeTL Group, imeng’ara katika Tuzo za Rais za Mzalishaji Bora wa Mwaka 2015 baada ya kutwaa tuzo tatu katika hafla iliyofanyika Hoteli ya Serena, Dar es Salaam. Tuzo hizo huandaliwa na Shirikisho la Viwanda Nchini (CTI) na mwaka jana zilishirikisha zaidi ya kampuni 350.
Katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na Rais, John Magufuli, MeTL inayoongozwa na Rais na Mkurugenzi Mtendaji, Mohammed `Mo’ Dewji ilitwaa tuzo kupitia kampuni zake za Star Oils (T) Ltd inayohusika na bidhaa za petroli, East Coast Foods & Fats inayozalisha bidhaa kadhaa ikiwa ni pamoja na mafuta ya kula iliyokipa tuzo kiwanda hicho, na kiwanda cha nguo cha 21st Century cha Morogoro.
Tuzo za mwaka huu zilihudhuriwa na watu takribani 300 kutoka sekta binafsi na taasisi za serikali ikiwemo wafanyabiashara wakubwa pamoja na wataalamu mbalimbali. MeTL Group yenye utajiri wa zaidi ya dola bilioni 1 (Sh trilioni 2.2) na inayoongoza kwa kutoa ajira upande wa sekta binafsi ikiwa imeajiri watu 28,000 kwa Tanzania pekee, ilianzishwa mwanzoni mwa miaka ya 1970 na Gulamabbas Dewji na tangu hapo imekua kwa kasi kubwa kiasi cha sasa kuchangia asilimia 3.5 katika Pato la Taifa.
MeTL imejikita katika viwanda vya nguo, usagaji nafaka, utengenezaji wa vinywaji baridi, usindikaji wa mafuta ya kula, usindikaji wa chai, kilimo cha mazao mbalimbali yakiwemo mkonge, sekta ya nishati na kadhalika.
Akizungumza baada ya tuzo hizo, Dewji alisema amehamasika kuona kampuni yake inafanya vyema, huku akiahidi kuendelea kufanya kila linalowezekana kutanua kampuni zake ili aweze kuongeza ajira na hivyo kuisaidia serikali kupunguza tatizo la ajira kwa vijana na Watanzania kwa ujumla.
Chanzo Gazeti La Habari Leo

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa