Na
Ally Daud-Maelezo
Vijana
wameaswa kuacha kukaa majumbani na kusubiri fursa za maendeleo ziwafate walipo
na badala yake watumie muda mwingi kujishughulisha kwa kufuata fursa zilipo ili
kukabiliana na tatizo la ajira kwa vijana nchini.
Akizungumza
hayo wakati wa uzinduzi wa Kitabu cha taarifa ya utafiti wa Sauti za Vijana
Tanzania Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana ,Ajira na walemavu Mhe. Jenista
Mhagama amesema kuwa vijana wasikae majumbani na vijiweni kutegemea Serikali
iwapelekee fursa hizo.
“Vijana
tusikae majumbani na kushinda vijiweni tukitegemea kwamba tutawaletea fursa
huko mlipo , mnatakiwa mtoke na mtumie muda wenu kufikiri jinsi ya kujikwamua
na tatizo la ukosefu wa ajira kwa kutumia fursa zitolewazo” alisema Mhe.
Mhagama.
Aidha
Mhe. Jenista alisema kuwa Serikali
imeanza kutenga Shilingi Bilioni 15 kila bajeti kwa ajili ya kukuza ujuzi na
kujikwamua kiuchumi ili kuleta maendeleo kwa vijana na taifa kwa ujumla.
Mbali
na hayo Mhe. Mhagama aliunga mkono kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul
Makonda kwamba ni marufuku kwa kumbi za starehe na mahali popote kuuza kilevi
aina ya shisha kwani kinaharibu nguvu kazi ya vijana wa leo.
“Nasisitiza
tena marufuku kwa kumbi za starehe na
mahali popote kuuza kilevi aina ya shisha kwani inaharibu uwezo wa kufikiri kwa
vijana na kushindwa kufanya kazi matokeo yake uchumi wa nchi unazorota ,kwa
yeyote atayekiuka maagizo haya hatua kali zitachukuliwa juu yake.
Aidha
Mhe. Jenista aliwataka vijana kutumia vizuri fursa iliyotolewa na Serikali ya
awamu ya tano kwa kutoa Shilingi Milioni 50 kwa kila kijiji ili kuleta chachu
ya maendeleo kwa jamii na taifa kwa ujumla.
Mwisho.
0 comments:
Post a Comment