Na:
Frank Shija, MAELEZO
Wakonta
msichana aliyepata ajali ya gari amewaomba wa samaria wema kujitolea kumsaidia
ili aweze kutimiza ndoto zake za kuwasaidia watu wengine wenye matatizo
yanayofanana na tatizo lake kupitia uandishi wa Filamu na kuanzisha Taasisi
itakayosaidia kutoa mahitaji maalum kwa watu hao.
Ombi
hilo limetolewa na Msichana huyo Wakonta Mapunda alipokuwa akiongea na
waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari - MAELEZO leo Jijini Dar
es Salaam.
Wakonta
amesema kuwa kutokana na changamoto alizokumbana nazo baada ya kupata ajali
ikiwa ni pamoja na kutumia ulimi kuandika amejikuta akiwa muandishi wa Filamu
hivyo anakusudia kutumia ujuzi huo kusaidia watu wenye matatizo kama yake.
Amesema
kuwa lengo lake kubwa ni kuwa muandishi wa Filamu zitakazo waunganisha
jamii,kutia moyo na faraja zitakazo kuwa kiungo muhimu cha watu wenye uhitaji
maalum.
Ameongeza
kuwa katika kuhakikisha anatimiza malengo yake hayo amemekusudia kuanzisha
Tasisi itakayokuwa ikitoa misaada kwa na kuwawezesha watu wenye matatizo kama
yake katika kuwapatia mitaji na huduma za kijamii.
Aidha
ametoa wito kwa wadau mbalimbali wenye uwezo kifedha kuweza kushirikiana naye
katika kuanzisha Taasisi hiyo ili hatimaye watu wenye uhitaji maalum wapate
mahali pa kupatia misaada na huduma zao.
Akizungumzia
changamoto anazokabiliana nazo Wakonta amesema kuwa suala la gharama za
matibabu limekuwa kikwazo kikubwa kwake ambapo mpaka sasa anatakiwa kufanyiwa
kipimo cha CT Scan MRI katika hospitali ya Taifa Muhimbili ambacho kina gharama
kubwa.
Ameomba
wasamaria wema kumsaidi ili aweze kufanikisha kupata huduma hiyo ambapo alitaja
njia ya kumfikishia msaada huo kuwa ni Benki ya CCRDB Akaunti namba, Jina la
Akaunti Wakonta Kapunda, Akaunti na. 0152292436800, M-PESA 0755836896, Airtel
Money 0683886446 na TIGO PESA 0656771529
Kwa
upande wake Baba mzazi wa binti huyo, Brazilio Kapunda amesema kuwa wao kama familia wanamuunga mkono
mtoto wao katika kufika ndoto zake za kuwa muuandishi mahiri wa Miswada ya
Filamu na kuanzisha Taasisi itakayo kuwa inawasidia watu wenye mahitaji kama
yake.
Aliongeza
kuwa kwao ilikuwa ni mtihani mkubwa kwakuwa tukio hilo lilitokea pasipo
kutarajiwa
Awali
akitoa historia ya mkasa wake uliompelekea kukutwa na matatizo hayo alisema
ilikuwa ni tarehe 3 Februari 2012 siku ambayo walikuwa na mahafali ya kumaliza
kidato cha sita katika shule ya Sekondari ya Wasichana ya Korogwe, ndipo ajali
mbaya iliwakuta wakiwa wanafunzi tisa baada ya mwenzao mmoja kuingia ndani ya
gari la ndugu yake aliyekuja kumtembela na ghafla gari hilo lilianza kurudi
nyuma kwa kasi kubwa ndipo walipokutwa na majanga hayo.
“Hapo
ndio ilipokua mwanzo wa safari yangu ambayo sijawahi hata kuifikiria kwani
nilivunjika uti wa mgongo na kupooza kutoka mabegani mpaka miguuni. Nilifanyiwa
operation Muhimbili bila mafanikio.Nimekuwa mtu wa kukaa na kulala tu,muda
mwingi nimekuwa nautumia kuangalia Filamu ndipo alipojikuta ametamani kuwa
muandishi wa miswada ya Filamu”
Wakonta
amesema kuwa baada ya kuwa anaangalia Filamu kwa muda mrefu alijikuta navutiwa
na uigizaji wa msanii mmoja katika Filamu ya kihindi inayojulikana kwa jina la
“Like Stars from Heaven”ambapo mhusika mkuu alikuwa mtoto mwenye matatizo ya
ubongo alikumbana changamoto kadhaa hatimaye alifanikiwa kuonyesha kuwa kuna
kitu anaweza kufanya kwa manufaa ya jamii.
0 comments:
Post a Comment