Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akizungumza wakati wa kuhitimisha kikao cha kazi kilichodumu kwa siku
mbili ambao alipokea na kujadili masuala mbali mbali yanayohusu
mazingira, kulia ni Waziri Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia
Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba.
Waziri
Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira
Mhe. January Makamba akichangia jambo wakati wa kikao kazi cha Idara ya
Mazingira kilichoongozwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiwa kwenye picha ya pamoja na Watendaji wa Idara ya Mazingira na Wakuu
wa Vitengo, waliokaa pamoja na Makamu wa Rais kushoto ni Waziri Nchi
Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira Mhe.
January Makamba na kulia ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais
Ndugu Mbaraka Abdulwakil.
.............................. .............
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
amewataka watendaji wa Idara ya Mazingira katika ofisi yake wajipange
vizuri kwa ajili ya kufanya tathmini ya athari za kimazingira mjini
Dodoma wakati serikali ikijiandaa kuhamia kwenye mji huo.
Makamu
wa Rais ametoa kauli hiyo 21-Aug-16 alipokuwa akifunga mkutano wa kazi
wa siku mbili na watendaji wa Idara ya Mazingira ambapo walijadili namna
ya kukabiliana na uharibifu wa mazingira unaoendelea kote nchini.
Ameeleza kuwa hatua hiyo itasaidia kuuweka mji wa Dodoma salama kimazingira ikiwemo ubora wa miundombinu za maji taka.
Makamu
wa Rais amesema kutokana na idadi kubwa ya watu hasa watumishi ambao
watahamia Dodoma bila miundombinu imara hali ya uchafuzi wa mazingira
itakuwa si nzuri hivyo ni muhimu kwa watendaji hao kuweka mipango na
mikakati madhubuti ya kuhakikisha mji wa Dodoma hautaathirika
kimazingira.
Kuhusu
utendaji kazi wa watumishi wa ofisi yake amewataka watumishi wote
kufanya kazi kwa ushirikiano na kwa uwazi katika matumizi ya fedha za
miradi na hasa inayohusika na uhifadhi wa mazingira jambo ambalo litaondoa manung'uniko miongoni mwa watumishi na wananchi kwa ujumla.
Amesema
ushirikiano huo miongoni mwa watumishi utasaidia kwa kiasi kikubwa
ufanisi katika kazi za kila siku ili kufikia malengo waliyojiwekea.
Makamu
wa Rais amesema ataendelea na utaratibu wa kukutana na watumishi kila
baada ya miezi 4 katika ngazi ya viongozi kama hatua ya kujitathmini
katika mipango ya kazi waliyojiwekea.



0 comments:
Post a Comment