Na Adili Mhina
Tume ya Mipango imekamilisha zoezi la kuandaa wataalamu wanaotarajiwa kutoa mafunzo juu ya usimamizi na utayarishaji wa miradi ya uwekezaji katika sekta ya umma kwa maofisa wa serikali walio chini ya Idara za Sera na Mipango na zile za Uwekezaji katika Wizara, Mikoa, Halmashauri, Mashirika pamoja na Taasisi mabalimbali za Umma hapa nchini.

Akifunga mafunzo hayo mwishoni mwa juma, Naibu Katibu
Mtendaji kutoka Tume ya Mipango anayesimamia Klasta ya Biashara za
Kimataifa na Mahusiano ya Uchumi, Bw. Paul Sangawe alisema kuwa katika
awamu hii ambapo Shilingi trilioni 59 kati ya trilioni 107 zinatarajiwa
kutolewa na Serikali pekee katika kutekeleza Mpango wa Pili wa Maendeleo
wa Taifa wa Miaka Mitano, Serikali imeamua kujipanga upya ili
kuhakikisha miradi yote itakayoanzishwa inaleta tija kwa wananchi.
“Tumeamua kujiandaa mapema kwa sababu tunatarajia miradi
mingi mikubwa itaanzishwa katika kipindi hiki cha utekelezaji wa Mpango
wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (FYDP II). Hivyo, ni
muhimu huko mtakapoelekea kutoa mafunzo mhakikishe mnatoa mbinu sahihi
za kukabili changamoto zinazojitokeza katika kutayarisha, kutekeleza na
kusimamia miradi ya maendeleo”, Alisema Bw. Sangawe.
Sangawe aliongeza kuwa baada ya mafunzo hayo kuwafikia
walengwa wote hakutakuwa na sababu kwa maofisa wa serikali kushindwa
kuandaa, kutekeleza, kusimamia au kutoa ushauri sahihi pale serikali
inapofanya uwekezaji kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Akitoa neno la shukrani kwa uongozi wa Tume ya Mipango kwa
niaba ya wahitimu wote, Mchumi Mwandamizi kutoka Ofisi ya Rais, Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bi. Sauda Ponda alisema kuwa
wahitimu wote walipata fursa ya kujadili, kuuliza na kufanya mazoezi
mbalimbali katika vikundi kwa lengo la kuongeza uelewa na kuimarisha
uwezo kwa ajili ya kwenda kutoa mafunzo kwa wahusika.
“Kwa niaba ya wenzangu wote napenda kutoa shukrani za pekee
kwa Tume ya Mipango kwa kuandaa mafunzo haya, waalimu wetu kutoka Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam wametufundisha vizuri na wametupa mazoezi ya
kutosha na sote tuko tayari kwenda kutoa elimu hii kwa wenzetu,”.
Alisema Bi. Ponda.
Wataalamu hao waliotumia siku tano kuchambua kwa kina
Mwongozo wa Usimamizi na Utayarishaji wa Miradi ya Uwekezaji katika
sekta ya Umma ambao ndio unaopaswa kufuatwa katika kutekeleza miradi
yote ya serikali, wanatarajiwa kugawanyika katika makundi mbalimbali
yatakayotoa mafunzo kikanda ambapo zoezi hilo litaanza tarehe 22 mwezi
huu.
---MWISHO---
Captions
DSC03047: Mchumi Mwandamizi kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bi. Sauda Ponda akitoa neno la shukrani kwa uongozi wa Tume ya Mipango kwa niaba ya wahitimu.
DSC03053: Naibu Katibu Mtendaji kutoka Tume ya Mipango anayesimamia Klasta ya Biashara za Kimataifa na Mahusiano ya Uchumi, Bw. Paul Sangawe akifunga mafunzo ya kuandaa wataalamu wa kufundisha masuala ya Usimamizi na Utayarishaji wa Miradi ya Uwekezaji katika sekta ya Umma, pembeni yake ni Kaimu Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango anayesimamia Klasta ya Uchumi Jumla, Dkt. Lorah Madete.
DSC03062: Wajumbe wa mafunzo wakimsikiliza Naibu Katibu Mtendaji kutoka Tume ya Mipango anayesimamia Klasta ya Biashara za Kimataifa na Mahusiano ya Uchumi, Bw. Paul Sangawe wakati wa kufunga mafunzo hayo.
___________
Adili Justine Mhina,
Information Officer,
Ministry of Finance and Planning,
Planning Commission,
Box 9242,
Dar es Salaam.
Tel 2112681-4/2127122
Fax 2115519/2117103
Mob 255-787 677 881

0 comments:
Post a Comment