Na Godfriend Mbuya
Baraza
la Taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi nchini (NEEC)
limewatahadharisha wananchi juu ya uwepo wa taasisi au watu binafsi
ambao wanawadangaya kuwa mpango wa milioni hamsini katika kila kijiji
fedha zimetoka na watoe fedha ili kuzipata.
Akizungumza katika kipindi cha SUPAMIX kinachorushwa na East Africa Radio, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Bengi Issa
amesema serikali bado inaendelea na mchakato wa fedha zilizoahidiwa na
Rais Dkt. John Magufuli haujakamilika na ukikamilika wananchi
watajulishwa.
“ Serikali bado inaendelea na utaratibu wa mpango huu na utakapo kamilika watataarifiwa” Amesema Bengi.
Aidha
Bengi ametoa onyo kwa watu binafsi na vikundi ambavyo vinadanganya
wananchi wachangie fedha ili kupata fedha hizo watachukuliwa hatua kali
za kisheria.
Ikumbukwe
kuwa wakati wa uchaguzi wa mwaka jana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania aliahidi kutoa milioni 50 kila kijiji ili wananchi waweze
kunufaika kupitia fedha hizo kwa kufanyia miradi ya maendeleo.
0 comments:
Post a Comment