Home » » Dhamira ya mtu ndiyo inaweza kataa madawa ya kulevya -Dudu Baya

Dhamira ya mtu ndiyo inaweza kataa madawa ya kulevya -Dudu Baya


Na Godfriend Mbuya

Msanii wa Bongo Flava Dudu Baya amesema ili mtu aweze kuacha madawa ya kulevya ni hadi dhamira yake imsute na kuamua mwenyewe kwa dhati.

Akizungumza katika kipindi cha FNL kinachorushwa na EATV ,Dudubaya amesema msanii mwenzake Chid Benz na wasanii wengine hawawezi kuacha kutumia madawa ya kulevya kwa watu kuwapeleka popote kama dhamira yao haijawasuta kuhusu jambo hilo.

“Kama una mtoto ambaye ni changudoa hata ufanye nini kama dhamira yake haijamsuta akaamua kwa dhati kutoka moyoni mwake hataacha atakuwa anaruka hadi ukuta ndivyo ilivyo kwa watu ambao wameshajiingiza kwenye madawa ya kulevya” Amesema Dudu Baya.


Aidha Dudu Baya amemsifu msanii Mr. Nice kwa kuendelea kushiriki 'show' mbalimbali za muziki nchini Kenya ambapo anafanya vizuri na kuwataka wasanii wengine kutong'ang'ania nchini wakati sehemu nyingine wanaweza kufanya vizuri zaidi.

Pamoja na hayo Msanii huyo amewataka wasanii nchini kutokubali kudharauliwa na baadhi ya watu kwa kulipwa ujira mdogo katika kazi ngumu ambazo wanafanya kwakuwa kwa kufanya hivyo kunazidi kushusha thamani yao.

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa